Marekani yasimamisha matumizi ya F35

Tume ya pamoja ya Marekani na washirika wake wasimamisha matumizi ya ndege za kivita aina ya F35 B kutokana kuwa na matatizo ya kiufundi

Marekani yasimamisha matumizi ya F35

Baada ya wiki iliyopita ndege ya kivita F35B kuanguka kusini mwa jimbo la Karolina nchini Marekani, Nchi hiyo pamoja na wshirika wake wamesimamisha matumizi ya ndege hizo ainaya F35.

Msemajı wa mpango wa kuhabarisha wa pamoja bw  Joe Dellavedova alisema,

"Wakati mfumo wa mabonma ya mafuta ukichunguzwa katika ndege za F35, Marekani na washirika wake wote tumesimamisha matumizi ya ndege hizi"

Maamuzi hayo yamefikiwa baada ya tar 28 mwezi wa 9 karibu na eneo la Beafort moja ya ndege hizi za kivita F35B kuanguka mara baada ya matokeo ya awali ya uchunguzi kuanza kutolewa.

Alisema Dellavedova kwamba chanzo cha ajali hio ni kifaa katika mfumo wa mabomba ya nishati,mafuta, vifaa hivyo vitabadilishwa na ndege zote ambazo zitakuwa hazina matatizo tena katika mfumo huo wa mafuta zitarudi,kufanya kazi kama kawaida.

Alifahamisha kwamba hii ilikuwa ajali ya kwanza ya ndege hizi za kivita F35 ambazo zinauwezo wa kupaa na kutua kiwima wima katika ndege hizo inasemekana kuna matatizo mengi ya kiufundi.

Mnamo mwezi wa kumi mwaka 2016 ndege ya  aina hii hii F35 Iliwaka moto injin yake na kusababisha rubani wa ndege hio kuitulisha kwa dharura, ambapo kwa taabu sana rubani alifanikiwa kuokolewa.

Jeshi la Marekani kwa mara ya kwanza lilitumia aina ya ndege hii ya kivita kufanya mashambulizi ya anga kwa eneo lilikouwa linasadikiwa kuwa ni la taleban nchini Afghanistani mnamo mwezi uliopita. 


Tagi: F35B , Marekani

Habari Zinazohusiana