Khamenei afafanua kauli yake

Ali Khamenei afafanua kauli yake ya inatubidi tuzigeuzie nyuso zetu mashariki

Khamenei afafanua kauli yake

Kiongozi wa kidini wa Taifa la Iran Ayetullah Ali Khamenei amesema nchi yake inapaswa kugeukia  mataifa ya Asia ambayo ndiyo yameonyesha kupiga hatua kubwa kwenye sayansi.

Katika taarifa ya maandishi iliyotolewa na ofisi yake kiongozi huyo alikutna na wana sayansi, wana taaluma,waelemishaji na wanafunzi wenye mafanikio mjini Tehran.

Alisema watuwaliofanikiwa kielimu inapaswa waiunge mkono serikali, kwamba watu hawa wasaidie katika kudumisha uhuru wa nchi, haki sawa, maendeleo pamoja na kutatua matatizo ya kijamii

"Nchi lazima ifaidike kutoka kwa wasomi, kama Kielimu hatutaendelea vitisho kutoka kwa maadui zetu mara zote vitatukabili". alisema.

 

 

" Inatubidi kujenga mahusiano na zilizopiga hatua kielimu. Na nyingi ya nchi hizi zipo katika bara la Asia. Kwa ajili hiyo basi nyuso zetu tuzielekeze mashariki, sio magharibi. Kuangalia Ulaya pamoja na magharibi zaidiya  kupitwa na wakati na kujishusha hakuna faida nyingine yeyote" alisema Khameney.Habari Zinazohusiana