Washington Post yachapisha makala ya mwisho ya Jamal Kashogghi

Jarida la Washington post lachapisha sehemu ya mwisho ya makala ya Jamal Kashoghi

Washington Post yachapisha makala ya mwisho ya Jamal Kashogghi

Majira ya jioni Jumatano jarida la Washington Post lilichapisha sehemu ya mwisho ya  makala ya Jamal Kashogghi, mwandhishi ambaye  hajulikani alipo tangu alipoonekana akiingia kwa mara ya mwisho katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul.

Katika makala hiyo ambayo ilikuwa na kichwa cha habari " Kitu ambacho ulimwengu wa kiarabu unakihitaji zaidi ni uhuru wa kujieleza".

Khashogghi aliandika kuhusu uhuru wa vyombo vya habari katika  mataifa ya kiarabu.

Aliandika makala hio baada ya kuona ripoti iliyoandaliwa na asasi moja ya kiraia nchini Marekani, Freedom House  kuhusu uhuru duniani mwaka 2018 "2018 Freedom in the World".

Hakupendezwa na alichokiona kwenye makala hayo.

" Kuna nchi moja tu katika nchi za kiarabu ambayo imewekwa kwenye kundi la nchi huru . Nchi hiyo ni Tunisia.

Nchi za Jordan, Moroko na Kuwait zimewekwa katika kundi la nchi zenye uhuru kiasi wa wastani . Nchi nyingine zote zilizobaki  hakuna uhuru.

Kutokana na utafiti huo Kashogghi aliandika mambo mengi kuelezea hali hiyo na athari zake.

Mwishoni alitoa mapendekezo yake kwamba mataifa ya kiarabu yanahitaji aina mpya ya vyombo vya habari vya kimataifa ili wananchi wa mataifa hayo wapate kufahmu yanayo endelea duniani.

Khashogghi anahofiwa kuuawa, baada ya kuingia katika ubalozi mdogo wa Saudia jijini Istanbul Oktoba 2.

Siku hiyo hiyo wasaudia wengine 15, kati yao maafisa wa nchi hiyo waliwasili Istanbul kwa ndege mbili na kutembelea ubalozi wakati Khashogghi akiwa bado ndani ya ubalozi huo, maelezo hayo ni kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya jeshi la  Polisi  Uturuki.

Watu wote 15 imefahamika waliondoka  kutoka Uturuki.

 Habari Zinazohusiana