Rais Erdoğan kuzungumzia sakata la Khashoggi kwa undani Jumanne

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğana kuzungumza kwa undani zaidi kuhusu sakata la Jamal Khashoggi

Rais Erdoğan kuzungumzia sakata la Khashoggi kwa undani Jumanne

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğana kuzungumza kwa undani zaidi kuhusu sakata la Jamal Khashoggi.

Rais wa Uturuki atarajiwa kuzungumzia kwa kina  kuhusu sakata  la mwanahabari  Jamal Khashoggi ambae alipotea baada ya kuonekana  kwa mara ya mwisho akiingia katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul.

Rais Erdoğan atazungumza kwa kida kuhusu sakata la Jamal Khashoggi Jumanne Oktoba  23.

Hayo rais Erdoğan ameyazungumza Jumapili katika uzinduzi   wa njia mpya ya metro mjini Istanbul.

Rais Erdoğan amesema  kwanini watu 15 kutoka Saudia wamekuja  Uturuki kwa wakati mmoja  wakati ambapo Khashoggi alikuwa mjini Istanbul.

Rais wa Uturuki amehoji pia kwanini wakamatwe watu wengine 18 nchini Saudia.

Saudia imekiri  Jumamosi kuwa mwanahabari Jamal Khashoggi aliuawa katika ubalozi wa mdogo wa Saudia  baada ya ugomvi ulizuka baina yake na maafisa katika ubalozi huo.

Mfalme wa Saudia amewafuta kazi maafisa wa ngazi za  juu ikiwemo Ahmad Hassan Mohammad Asiri ,  mkurugenzi msaidizi wa idara ya  upelelezi Saud al Qartani baada ya sakata la Khashoggi kuibuka.Habari Zinazohusiana