Rais Erdoğan atajwa kama muislamu mwenye ushawishi zaidi duniani

Rais Recep Tayyıp Erdoğan atajwa kama muislamu mwenye ushawishi mkubwa zaidi ulimwenguni

Rais Erdoğan atajwa kama muislamu mwenye ushawishi zaidi duniani

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan ameshika nafasi ya kwanza katika orodha ya waislamu 500 wenye ushawishi mkubwa duniani.

Orodha hiyo huandaliwa kila mwaka na taasisi ya "Jordan-based Royal Islamic Strategic Studies Centre", taasisi hii imekuwa ikandaa orodha hii tangu mwaka 2009.

Katika toleo lake la 10  , orodha kwa ajili ya mwaka 2019,  limechapishwa mwezi Oktoba mjini Amman nchini Jordan.

Katika matoleo yaliyopita ya kitabu hicho yanaonyesha mwaka 2016 na 2017 rais Erdoğan alishika nafasi ya 8, mwaka 2018 alishika nafasi ya 5.

Katika orodha ya mwaka 2019 mfalme wa Saudia Salman bin Abdul-Aziz Al-Saud alishirika nafasi ya pili, na nafasi ya tatu kuchukuliwa na mfalme wa Jordan Abdullah II Ibn Al-Hussein

Kitabu hicho lengo lake ni kutaja ushawishi walionao baadhi ya waislamu kwa "umma" ushawishi walionao kwa niaba ya umma.

Mshawishi wamemuelezea kama mtu yeyote ambaye ana nguvu  kiutamaduni, kiimani, kifedha, kisiasa, au nyingineyo au  kufanya mabadiliko ambayo yatakuwa na manufaa kwa jumuia ya waislamu  na dunia nzima.

 Habari Zinazohusiana