Dunia ni kubwa kuliko mataifa matano

Bila utaratibu unaozingatia haki hakutakuwa na amani wala usalama, Mkuu wa kitivo cha siasa chuo kikuu cha Yıldırım Beyazıt ,Ankara Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL anatufafanulia

Dunia ni kubwa kuliko mataifa matano

Karne ya ishirini ni karne ambayo iligubikwa na ukatili na unyama wa kila aina. Ni karne ambayo ndani yake kulikuwako na vita kuu mbili za dunia, katika vita hizo sio tu binadamu tu waliopoteza maisha, bomu la nyuklia lililotumika wakati huo lilisababisha viumbe hai wote waliokuwako eneo hilo navyo  kutokomezwa.

Taratibu zilizowekwa baada ya kumalizika vita kuu ya pili ya dunia hazikuwa kwa ajili ya kuzuia vita na madhara yake visijirudie tena au kwa ajili ya kulinda amani, bali zilikuwa ni kwa ajili ya kulinda maslahi na nafasi za wale  walioshinda vita hivi, Mfano ni mfumo wa Bretton woods ambao unaifanya dola ya Marekani kuwa sarafu ya msingi ya Dunia.

Umoja wa mataifa unatekeleza taratibu zilizowekwa na hawa washindi wa vita.

Mkuu wa kitivo cha siasa chuo kikuu cha Yıldırım Beyazıt ,Ankara Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL anatufafanulia...

Mfumo wa Breton Woods ambao kipindi cha vita baridi ulionekana ukifanya kazi vizuri hivi sasa unavuruga umoja wa mataifa.

Mgawanyo wa madaraka (nguvu) baina ya mataifa matano wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa; Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa na Uchina, umekuwa ukibadilika.

Kumalizika kwa vita baridi, kumepelekea viranja wakuu wa dunia wajaribu kudumisha utaratibu uliokuwapo kwa kutafuta kujiunga na miunganiko au ushirika tofauti tofauti wa kidunia

Ukitazama yaliyotokea Irak, Afghanistan, Boznia,Krimea na Siria utaona ni jinsi gani hii miunganiko ya kidunia jinsi imeundwa au jinsi haikuundwa dhahiri miunganiko hiyo haikuwapo kwa msingi ya kutenda haki. Utaratibu wa kidunia unaoweza kusema ni mwendelezo wa vita baridi,Vile kadiri siku zinavyoenda ndivyo unavyojionyesha wazi wazi na kufahamika, hivyo basi hata wapinzani wa taratibu hizi nao wamekuwa wakiongezeka.

Kuhusina na hili rais wa Uturuki Recep Tayyib Erdoğan mara zote kila akipata fursa amekuwa akipinga utatatibu uliopo kwa kusisitiza kwamba dunia ni kubwa kuliko mataifa matano.  

Teknolojia ya habari na mawasiliano ya kidunia imewezesha kadri siku zinavyozidi kwenda gharama za kudumisha jamii zilizojitenga au zisizotenda haki kuwa kubwa.

Utaratibu wa vita baridi hauwezi kufanikiwa katika ulimwengu huu wa sasa ambao kila aina ya habari unaweza kuipata kiurahisi na aina yeyote ya udhalimu kirahisi kabisa unaweza kuonekana.

Leo hii tunaishi katika kipindi ambacho hatuko salama. Tumefikia hatua ambayo dunia inabidi ibadili utaratibu ili tuwe salama au iendelee na utaratibu wa zamani tuangamie sote. Ndio, kudumisha utaratibu wa zamani gharama zake zinakuwa kubwa siku hadi siku.

Tofauti na wakati uliopita  viranja hawa wa dunia hivi sasa wana silaha kama mabomu ya hydrojeni na silaha nyingine za kikemikali, ambazo sio tu zinaweza kungamiza binadamu bali na viumbe hai vyote.

Katika hali hii iliyopo hivi sasa akitokea kiongozi wa kisiasa ambaye “hamnazo” katika mataifa haya viranja, inamaanisha dunia nzima na vilivyomo itakuwa katika hatari ya kutokomea.

Katika mazingira  ambayo utaratibu wa vita baridi unatiliwa mashaka lakini hakuna utaratibu mpya ambao unakubalika, basi inabidi uundwe ushirika ambao utahakikisha mataifa yote yananyang’anywa silaha hizi za maangamizi ili kulinda kizazi cha binadamu na viunmbe wengine na hatari ya kutokomea. Miunganiko hio ianzishwe kwa misingi ya haki, kwani haki huondoa udhalimu.

Na itafaa miunganiko hii iwepo katika kila pembe ya dunia kuweza kudumisha amani na utulivu.

Kwa ajili kudumisha na  kutenga haki inabidi kufikiria  miunganiko ya kimataifa na zaidi. Ili kuweza kudumisha amani na utulivu itakayonufaisha na vizazi vijavyo inabidi ianzishwe miunganiko inayozingatia haki katika kila ngazi na katika kila eneo. Wanataaluma, wafanya biashara, makundi ya kitaaluma, taasisi zisizo za kiserikali,wanafunzi,wanamichezo, wanasanaa kwa pamoja inabidi wawe sehemu ya miunganiko hii ya kihaki.

Katika kufanikisha haya inabidi watu washirikiane katika Nyanja mbali mbali, kama ni wanafunzi kama ni wafanyabiashara  wazidishe kushirikiana. Ni  katika kushirikiana wanaweza kupandisha sauti zao pamoja zikasikika.

Kipindi cha vita baridi katika hali ya kutoungana ilikuwa haiwezakani kupaza sauti kupitia vyombo vilivyokuwepo, Hivi sasa kutokana na maendeleo yaliyofikiwa katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano, watu wa fani mbali mbali kutoka nchi mbali mbali wanaweza kuanzisha ushirikiano. Lazima katika kila fani ziwepo juhudi za pamoja za kuanzisha ushirikiano.

Kiuhalisia hatari ipo karibu sana, matatizo ambayo ni ya kidunia hatuwezi kuyatatua katika hali za ubinafsi, basi bila kuzingatia dini, kabila, jinsia, rangi, au mtazamo, Hatari inayoikabali dunia ni hatari kwa kila binadamu hivyo basi ni lazima kuongeza juhudi katika kutafuta mashirikiano ya kihaki katika kila ngazi na kila nyanja. Tutumie akili zetu kuweza kukabiliana na janga lililopo.

Tutakapofanya hivi kidogo kidogo mwishowe tutafanikiwa, Mfano Marekani ilipojichukulia uamuzi peke yake wa kuitambua Yerusalem kama mji mkuu wa Izraeli, baraza la usalama na mataifa mengi yalipinga uamuzi huo kwa sauti moja.

Dunia nzima imesimama kulaani na kupinga vikali mauaji ya kikatili ya mwanahabari wa Saudia Jamal Khashoggi, matukio kama haya ni matukio yanayotoa matumaini.

Hivyo hivyo mashirikiano ya kihaki yanapaswa  yaanzishwe pia dhidi ya matatizo kama vile ya Ukanda wa gaza, Rohingya, Siria, haki za binadamu,chuki dhidi ya Uislamu, na ubaguzi.

Watu wote washirikiane kwa pamoja kupinga vita masuala haya waonyeshe msimamo mmoja dhidi ya udhalimu, dhidi ya ukoloni mamboleo, dhidi ya silaha za kikemikali dhidi ya ufashisti na dhidi ya unazi mambo leo. 

Katika kila ngazi, udhalimu inabidi uwekwe wazi. Na mifumo ya kihaki ya kidunia inabidi ichukue nafasi na hata kwa kutumia nguvu itakapobidi.

Bila kujali dini, kabila, imani, rangi, chama, mtazamo kama hatutaweza kuzuia dhulma kwa kushirikiana kwa ngazi ya kidunia basi dhulma itadumu milele, kwa sababu hakuna taifa moja au kundi moja la watu linaloweza kuzuia dhulma ya ngazi ya kidunia. Ni jukumu la dunia nzima kushirikiana kutokomeza dhulma.

Bado hakuna utaratibu mpya wa kidunia ulioanzishwa.Duniani bado tunaishi kwa mateso. Uwezo wa kuifanya dunia hii iwe sehemu isiyo na dhulma na kila mtu apate haki yake tunao.

Njia yeyote ya kutenda haki tutakayoamua kuifuata, inabidi juhudi za kumshirikisha kila mtu zichukuliwe.

Vinginevyo tutakuwa tunatengeneza dunia ambayo haina misingi ya haki, kama ilivokuwa wakati uliopita, au mmoja kati ya hao viranja wa dunia aamue kulipua mabomu ya kuangamiza halaiki na kuwaangamiza binadamu wote.  Hatua stahiki inabidi zichukuliwe kabla hatujachelewa.

Mkuu wa kitivo cha siasa chuo kikuu cha Yıldırım Beyazıt ,Ankara Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL anatufafanulia...


Tagi: Bretton , amani , Haki

Habari Zinazohusiana