Mji wa Faizabad nchini India wabadilishwa jina

Mji wa Faizabad unaopatikana katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India umebadilishwa jina na sasa utaitwa Ayodhya

Mji wa Faizabad nchini India wabadilishwa jina

Mji wa Faizabad unaopatikana katika jimbo la Uttar Pradesh nchini India umebadilishwa jina na sasa utaitwa Ayodhya.

Waziri mkuu wa jimbo la Uttar Pradesh Yogi Adityanath baada ya kutangaza kwamba jina la mji wa Allahabad limebadilishwa na kuwa Prayagraj alitangaza pia jina la Faizabad limebadilishwa na kuwa Ayodhya.

Ayodhya ni alama ya "heshima,kujivunia na ufahari " alisema Adatyanath, pia alikazia kwamba mji huo unahusishwa moja kwa moja na mfalme wa mji huo, Rama. hivyo hakuna yeyote ambaye atakayeweza kuwadhulumu.

Wahindu wa kiradikali wanasema mnamo karne ya 16 Hekalu la maombi ya kihundi liliojengwa na mfalme Rama lilivunjwa na waislamu na badala yake wakajenga msikiti. Waislamu nao wametete kwamba hakuna ushahidi wowote unaoonyesha kwamba kulikuwa na hekalu la kihindu eneo hilo.

Wahafidhina wa kihindu wanataka lijengwe hekalu la kihindi katika ardhi hiyo. Mwaka 1992 wahindu wenye msimamo walivunja msikiti uliodumu tangu karne ya 16, tukio lililosababisha umwagajiwa damu mkubwa kwani zaidi ya watu elfu mbili wanaripotiwa walipoteza maisha.

 Habari Zinazohusiana