Uislamu na changamoto zake barani Ulaya

wakristo na wayahudi hata wasio na dini inabidi wawaunge mkono waislamu kwani uislamu ukifutika Ulaya hakuna atakaye nufaika

Uislamu na changamoto zake  barani Ulaya

Kwa muda sasa barani Ulaya kumekuwa na malumbano juu ya Uislamu. Malumbano haya licha ya kuwa ni dhidi ya waislamu, wahusika wakuu wa malumbano haya ni mataifa ya Ulaya, taasisi za ulinzi, wasomi wa kimagharibi pamoja na waandishi.

Mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Yıldırım Beyazıt cha mjini Ankara Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL anatufafanulia mada hii...

Malumbano haya si kwamba hayana msingi wowote.Utandawazi husababisha watu wa utambulisho,tamaduni,dini na lugha tofauti waingiliane na kuishi pamoja. Kuishi pamoja kwa mataifa kama Utawala wa Otoman si suala geni, lakini kwa mataifa ya magharibi ni suala geni.

Tunaweza kusema katika karne zilizopita mataifa ya magharibi yalifanya mahusiano ya kidini na kitamaduni na mataifa mengine kwa mtindo wa mtawala na mtawaliwa, Lakini kipindi hiki  wahamiaji wanapoelekea kwenye mataifa ya magharibi, Mataifa haya yanakutana na changamoto mpya.

Zama hizi inakuwa ni vigumu zaidi kuweza kuzikubali tofauti na kuishi pamoja watu kwa vile hizi ni zama mpya za mataifa huru,  tena binafsi na yenye tawala za serikali kuu.

Utamaduni wa Ulaya unaoendana na Uislamu

Ni hakika kwamba pale watu wa historia, dini na tamaduni tofauti wakiishi pamoja, matokeo yanayozaliwa kutokana na mwingiliano huu huyagusa mataifa, taasisi na wasomi.Unapozungumzia uislamu barani Ulaya haimaanishi desturi za kiislamu kutoka nje ya Ulaya bali desturi za ndani ya ulaya zinazofungamana na Uislamu. Ili uelezee uislamu ndani ya ulaya inabidi uonyeshe athari za uislamu katika dini, utamaduni na nyanja nyingine za maisha barani Ulaya. Ingawa itikadi ya kiislamu ni moja lakini kuna utofauti katika utekelezaji wa dini hii kulingana na eneo.

Uislamu wa Uturuki ukilinganisha na mashariki ya kati ukilinganisha na nchi za balkani kunakuwa kuna tofauti ndogo ndogo zinazotokana na mila na desturi za eneo husika.

Katika mtizamo huo basi hata kwa waislamu wa Ulaya haitakiwi wafuate tamaduni zote za waislamu wahamiaji. Ili mradi misingi mikuu ya Uislamu wanaitunza wafuate uislamu kulingana na Utamaduni, Uelewa na jeografia ya Ulaya.

Kama vile isivyokubalika ikitokea unaletwa utamaduni, sanaa, uelewa, fasihi  mpya katika nchi za Afrika, mashariki ya mbali au Uturuki hata Ulaya pia haitakubaliki ikitokea mtu akitaka kujaribu kubadilisha mambo haya.

Hili linabidi lieleweke. Kutokubalika huko hakutokani na kwamba labda utamaduni ni potofu, bali inatokana na kwamba kila jamii ina elimu na tamaduni inayofungamana na eneo la kijiografia inalopatikana.

Katika jamii zilizostaarabika ukiachilia mbali desturi ambazo zinafanana maeneo yote kikawaida kila jamii hupambana kuhakikisha utamaduni na mila zake zinadumu.

Tamaduni za Ulaya zinazofungamana na Uislamu ni suala ambalo wageni wanaokuja Ulaya pamoja na wenyeji wa Ulaya inabidi walifikirie. Tunaposema tamaduni za Ulaya zinazofungamana na uislamu tunamaanisha, Baadhi ya vipengele vinavyopatikana katika tamaduni za Ulaya kama ubaguzi wa rangi, ufashisti, unazi na mambo mengine kama hayo inabidi yaachwe.

Baadhi ya mambo yanayotiliwa mkazo kuhusiana na uislamu barani ulaya ni kwamba, wahamiaji wanaohamia Ulaya hawawezi kuwa na haki za binadamu , usawa, uhuru, vyama vingi, kuishi pamoja na desturi nyingine za msingi, hawawezi kuwa sawa na watu wa Ulaya. Ingawa inaweza kusemwa miaka ya hivi karibuni watu wenyewe wa Ulaya wamekuwa wakipuuza desturi hizi za kibaguzi.

Tabia ya kuwachukulia wahamiaji kama vile sio watu , ongezeko la wahamiaji na ubaguzi dhidi ya uislamu ndio vitu vya kwanza kuja akilini. Katika utafiti uliofanywa kuhusiana na mtazamo wa umma ni kwamba kiasi cha kutokubali mtu aliyetofauti nasi, Uoga dhidi ya vitu vilivyotofauti, mfanyakazi mwenzio ambaye yuko tofauti na wewe au jirani mnaye tofautiana,kwa kiasi kikubwa kimeongezeka.

Mtizamo wa Uislamu wa Ulaya unaojali usalama zaidi ya uhuru.

Unapotazama maandiko na matendo ya nchi za magharibi inaonekana  malumbano haya kuhusu Uislamu barani Ulaya hayajajikita zaidi katika uraia,tamaduni na desturi.  Mataifa haya ya Ulaya Mtizamo wao juu ya malumbano haya umejikita zaidi kwenye suala la usalama.

Ni kwa sababu hiyo kazi hii imejikita zaidi katika masuala yahusuyo usalama na sio tamaduni, kuishi pamoja, vyama vingi au utofauti.

Kukiwa na suala la kiusalama, bila shaka tahadhari za kiusalama zitachukuliwa. Hilo sio suala la kubishana.Lakini kuyaangalia masuala haya yanayohusu uraia, jamii,utamaduni,siasa, yanayowagusa mamilioni ya watu kwa mtizamo wa kiusalama pekee ni kulizidisha tatizo.

Ni suala linaloeleweka na kuhitajika kwa serikali yeyote, yanapotokea masuala mapya kuunda tume za kushuhulika na mambo hayo Lakini ili juhudi hizi ziweze kukubalika vizuri zaidi inabidi tume hizi zijielekeze katika kuelewa na sio kukandamiza, kubadilisha au kupiga marufuku.

Kwa  sababu hiyo mataifa ya Ulaya yanapounda tume kwa ajili ya kushuhulika na masuala ya Uislamu badala ya kujaza tume hizo na majina ya watu wasiokuwa waislamu wasioelewa chochote kuhusu Uislamu, Ingefaa zaidi tume hizi ziundwe na waislamu wenyewe. Katika hali hiyo tume  hiyo itakuwa imejikita zaidi katika mtizamo wa  asasi za kiraia na sio asasi ya kiusalama

.Majukumu ya waislamu…

Kuhusiana na Uislamu barani Ulaya, Kusema kwamba waislamu wametekeleza majukumu yao huku nchi zinahosika na waislamu wao ndio zikikosolewa sio haki.

Kama katika nchi za magharibi kuna matatizo yanayohusiana na elimu ya waislamu,uchumi,siasa, kujihusisha na elimu, matukio ya kihalifu kuongezeka pamoja na uwezo mdogo wa kufanya kazi matatizo haya ni waislamu wenyewe pamoja na serikali zao.

Pia ni muhimu wayaonyesha matatizo ya uwakilishi na haki ya kusema katika nchi hizo wanazotoka. Mwishowe huku wakifanya kazi kwa karibu na uongozi wa nchi husika, kwa mahusiano ya moja kwa moja na ya wazi,Inatarajiwa zifanyike juhudi za kuondoa mazingira ya vitisho na yanayotengeneza vitisho.

Kijamii Ulaya itapata faida gani ikiondoa Uislamu?

Baadhi ya sehemu za Ulaya zinataka uislamu au waislamu wasiokuwa na kasoro wanaopenda familia, na jamii .

Lakini ukilinganisha Ulaya na maeneo mengine ni Ulaya ambapo familia zilizoparaganyika, mapenzi ya jinsia moja, watoto waliotelekezwa, matumizi ya madawa ya kulevya na mambo mengine kama hayo yameenea zaidi. Ulaya imepoteza kwa kiwango kikubwa sana maadili mema.

Kutokana na uchumi kuwa mkubwa na watu kuridhika, watu hawa wanashindwa kuanzisha mahusiano yenye tija. Katika mazingira haya Ulaya ni Uislamu peke yake ndio ngome ambayo haijatetereka, Ulaya ikipoteza Uislamu haitapata faida yeyote zaidi tu ya kuharakisha anguko baya la bara hilo.

Wayahudi na Wakristo pia inabidi wawaunge mkono waislamu

Waislamu wakiwa katika hali ya kudhulumiwa hakuna faida yeyote inayoweza kupatikana kwa jamii nyingine, tulishaona wakati wayahudi na wakristo walipoiishi mazingira ya namna hiyo.

Maadili ya kijamii yanaopoporomoka kwa kiasi hicho, tabia zinapoharibika na Ubinafsi wa kupitiliza ni vitu ambavyo hata wakristo na wayahudi vitawadhuru, vile vile hata watu wasio na dini nao watadhurika .

Hivyo basi ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kwamba desturi na maadili yanalindwa kwa manufaa ya kila mmoja hasa hasa wakristo na wayahudi.

Ni jukumu la Waislamu wa Ulaya kufahamu kwa undani ajenda yao

Yote kwa yote ,Waislamu, wawe wa Afrika, wa Amerika, wa China, wa India, wa mashariki ya Kati na bila shaka wa Ulaya pia wote kwa pamoja inabidi wafahamu kiundani ajenda yao. Ni kivipi wataifahamu?, tuendelee wiki ijayo.

Mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Yıldırım Beyazıt cha mjini Ankara Prof. Dr. Kudret BÜLBÜLHabari Zinazohusiana