Maombi ya uwaziri kwa njia ya mtandao

Watano kati ya waliopitishwa kushika nyadhifa za uwaziri nchini Iraki walituma maombi ya nyadhifa hizo kwa njia ya mtandao

Maombi ya uwaziri kwa njia ya mtandao

 

Waziri mkuu wa Irak Abdulmehdi ametangaza kwamba kati ya mawaziri 14 waliopitishwa na bunge la nchi hio mawaziri watano walituma maombi yao kwa njia ya mtandao.

"Kati ya mawaziri 14 waliopitishwa na bunge mawaziri 5 walituma maombi yao kwa njia ya mtandao" ilisema taarifa.

Taarifa hiyo haikuwataja mawaziri hao 5 ni kina nani.

Waziri mkuu Abdulmehdibaada ya kushinda uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Mei na kuunda serikali, Oktoba 8 alitangaza yeyote aliyekuwa anataka kuwa waziri wa serikali hio atume maombi yake kwa njia ya mtandao.
 Habari Zinazohusiana