Rais Trump amtolea uvivu rais Macron

Kuhusiana na wazo linalotaka Ulaya ianzishe jeshi lake lisiloitegemea Marekani lililotolewa na rais Macron, rais Trump naye asema yake

Rais Trump amtolea uvivu rais  Macron

Rais wa Marekani Donald Trump amejibu pendekezo la rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ya kutaka nchi za Ulaya ziunde jeshi lake binafsi ili ziweze kujilinda dhidi ya Marekani, China na Urusi.

Ikiwa hivi karibuni atajielekeza mjini Paris katika maadhimisho ya miaka 100 ya kumalizika kwa vita kuu ya kwanza ya dunia, rais Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter yafuatayo kumlenga Macron.

"Kuhusu alicho kisema raisi Macron kwamba Ulaya inabidi iunde jeshi lake kujilinda dhidi ya Marekani, China na Urusi ni matusi. Labda Ulaya ilipe deni lake  kwanza kwa NATO ambayo Marekani inaifadhili kwa kiwango kikubwa".

Rais wa Ufaransa, Macron, katika taarifa aliyoitoa wiki hii jijini Paris aligusia kuhusu hatari inayoweza kutokana na Urusi, alisema Ulaya haitakuwa salama kama mpaka pale itakapokuwa na jeshi lake huru lisiloitegemea Marakani.

 Habari Zinazohusiana