Uturuki yataka mabadiliko katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa

Uturuki yatolea wito nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kwamba yafanyike mabadiliko katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa

Uturuki yataka mabadiliko katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa

Ijumaa hii Uturuki iliwaambia nchi wanachama wa Umoja wa mataifa kwamba umoja huo unapaswa kuwa wenye uwazi, wa kidemokrasia, unaowakilisha nchi zote na pia wenye kuwajibika.

Hayo yalisemwa na balozi wa kudumu wa Uturuki katika umoja wa mataifa Feridun Sinirlioğlu katika baraza la usalama lililoitwa  Kudumisha Amani na Usalama  kimataifa “Maintenance of International Peace and Security"

"Kadiri jinsi baraza hili litakavyokuwa likiendesha shughuli zake kwa uwazi ndivyo litakavyoonyesha uwajibikaji" alisema Sinirlioğlu.

Aliongeza kwamba baraza ambalo litajibu ipasavyo mahitaji ya nchi wanachama litakuwa bora zaidi katika dunia hii tete.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan amekuwa akipagania kwa muda mrefu yafanyike mabadiliko katika mfumo wa baraza la Usalama la umoja wa taifa kwa kutumia msemo usemao " Dunia ni kubwa kuliko mataifa matano"
 Habari Zinazohusiana