Waziri wa uchukuzi wa Uingereza ajiuzulu wadhifa wake

Waziri wa uchukuzi wa Uingereza Jo Johnson ajiuzulu wadhifa wake akipinga Brexit

Waziri wa uchukuzi wa Uingereza ajiuzulu wadhifa wake

Waziri wa uchukuzi wa Uingereza Jo Johnson ajiuzulu wadhifa wake  Ijumaa, akifahamisha kuwa haungi mkono mpango wa waziri mkuu Theresa May kujiondoa Umoja wa Ulaya (Brexit).

Johnson alichapisha makala mtandaoni akisema hatapiga kura kuunga mkono mpango ambao May ataufikisha bungeni, atakachokifanya ni kupigia debe iwepo kura ya maoni ya mara ya pili kuhusu mpango wa Brexit.

" Nikwa naandika makala hii ni kwa upande wangu ni dhahiri kwamba makubaliano haya yanayofanyika huko Brussels na Whitehall yatakuwa ni makosa makubwa mno" alisema.

Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje mstaafu ambaye pia ni kaka wa Johnson na mbunge wa Orpington alisisitiza kwamba makubaliano yatakayoafikiwa yataiacha Uingereza ikiwa dhaifu kiuchumi, pia haitakuwa na la kupinga katika masuala yanayohusu sheria za Umoja wa Ulaya ambazo ni lazima izifuate, na miaka mingi ya tashwishwi za kibiAshara " kama waziri wa uchukuzi nafahamu kwamba suala hili litasababisha madhara makubwa  kwa taifa letu"

Baraza la mawaziri la May lilisha athirika baada ya kujiuzulu kwa makatibu wa mambo ya nje na Brexit, Boris Johnson na David Davis.

Uingereza inategemewa kujitoa kabisa katika Umoja wa Ulaya Machi 29,2019.

 Habari Zinazohusiana