Rais Trump aendelea kumuandama Macron

Asema tatizo la Macron amepoteza mvuto miongoni mwa Wafaransa

Rais Trump aendelea kumuandama Macron

Rais Marekani Donald Trump arudi tena kwenye kurasa zake za mtandao wa kijamii Twitter Jumanne hii, akizidi kumuandama Macron, rais wa Ufaransa, safari hii akidai kwamba Macron amepoteza mvuto miongoni mwa wafaransa kutokana na kushindwa kutatua tatizo la ajira nchini humo.

"Tatizo ni kwamba Emmanuel amepoteza mvuto nchini Ufaransa, anakubalika kwa asilimia 26 na kukosesakan kwa ajira nchini humo ni karibu asilimia 10" alisema Trump . " Alikuwa anajaribu tu kudandia mada nyingine, niseme tu hakuna watu wazalendo kama wafaransa, kwani ni watu wanaipenda nchi yao na wako sawa".

Alionngeza rais Trump kwa kuakisi msemo wake wa kampeni " FANYA UFARANSA KUWA ADHIMU TENA"

Trump alikuwa amejielekeza kujibu hotuba iliyotolewa na Macron mwishoni mwa wiki kwenye kumbukumbu ya miaka 100 ya kumalizika kwa vita kuu ya dunia ambako Macron alizungumzia hatari ya sera ya utaifa kwanza ya uongozi wa rais Trump. 

Katika hotuba hiyo Macron alionya nchi ambazo zinatanguliza "maslahi yake kwanza", na kusema mashetani ya vita kuu ya kwanza ya dunia yanaweza kurudi tena kwa kitendo hicho.

Rais Trump akiendelea kujadili wazo la Macron kuunda jeshi huru la Ulaya ili kuilinda Ulaya dhidi ya Marekani, China na Urusi alisema, Macron ametoa wazo hilo lakini amesahau kwamba katika vita kuu ya kwanza na ya pili ya dunia ilikuwa ni Ujerumani ndio adui, na Paris walikuwa wameshaanza kujifunza kijerumani , Marekani ikagharamia NATO ambayo ikawaokoa wafaransa.

 

 


Tagi: Trump , Macron

Habari Zinazohusiana