Wakimbizi jamii ya Rohingya wasilazimishwe kurudi Myanmar

Mynamar na Bangladesh zitengeneze kwanza mazingira yatakayowezesha kurudi kwa warohingya kuwe kwa kibinadamu na pia salama

Wakimbizi jamii ya Rohingya wasilazimishwe kurudi Myanmar

Shirika la kimataifa la kutatua mizozo ambalo makao yake makuu yapo mjini Brussels (International Crisis Group, ICG) limetolea wito kwa Bangladesh kusitisha mpango wake wa kuwarudisha Myanmar wakimbizi wa jamii ya  Rohingya.

Katika taarifa ya taasisi hiyo iliyoitwa hatari za kurejeshwa  kwa lazima wakimbizi wa jamii ya Rohingya  "Bangladesh-Myanmar : The Danger of Forced Rohingya Repatriation", taasisi hiyo ilipinga makubaliano baina ya Myanmar na Bangladesh yanayohusu kuwarejesha zaidi ya wakimbizi wa jamii ya Rohingya 2,000  ifikapo Novemba 15.

Taasisi hiyo imeitaka pia UN na shirika lake la kuhudumia wakimbizi kuingilia kati suala hili kwa kulipinga waziwazi na kutumia ushawishi wake katika nchi zote hizo mbili kuzuia janga linaloweza kutokea kwa kuwarudisha kwa nguvu wakimbizi hao Myanmar.

 

 

 Habari Zinazohusiana