Mawaziri wapya wateuliwa baada ya baadhi kujiuzulu nchini Uingereza

Baada ya baadhi ya mawaziri kujiuzulu,Uingereza imeteua mawaziri wapya.

Mawaziri wapya wateuliwa baada ya baadhi kujiuzulu nchini Uingereza

Baada ya baadhi ya mawaziri kujiuzulu,Uingereza imeteua mawaziri wapya.

Steve Barclay ameteuliwa kama waziri mpya wa Brexit baada ya Dominic Raab kujiuzulu kufuatia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya.

Barclay ambaye anajulikana kwa sera zake zinazounga mkono kujiondoa kwa Uingereza  EU hapo awali alikua waziri wa afya.

Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Amber Rudd ametangazwa kama waziri mpya wa kazi  na kuchukua nafasi ya Esther McVey aliyejiuzulu siku ya Jumanne.

Mawaziri hao wawili walijiuzulu wakidai hawaziungi mkono sera za Theresa May kuhusiana na kujiondoa kwa Uingereza Umoja wa Ulaya.

Hata hivyo May anaendeela na mpango wake wa Brexit bila ya kujifikiria mara mbili.

 Habari Zinazohusiana