Washington Post yamtuhumu Trump kumtetea Bin Salman

Jarida la Marekani la Washington Post lamtuhumu rais Trump kumtetea mwanamfalme wa Saudia kuhusu mauaji ya Jamal Khashoggi

Washington Post yamtuhumu Trump kumtetea Bin Salman

Jarida la Marekani la Washington Post  lamtuhumu rais Donald Trump kutetea urongo wa  mwanamfalme wa Saudia Bin Salman  kuhusu mauaji ya mwanahabari Jmal Khashoggi.

Jarida hilo la Washington Post limesema kuwa rais Trump aanatupilia mbali hitimisho lililotolewa na idara ya  upelelezi ya Marekani  kutokana na kwamba mpango huo unakwenda kinyuem na matakwa yake ya kisiasa.

Taarifa hiyo  dhidi ya rais Trump kutoka katika  jarida la Washington Post imetolewa Jumapili Novemba  18.

Jarida hilo limechapisha taarifa ambayo  inafahamisha kuwa mwanamfalme wa Saudia  Bin Salman amejaribu  kujiondoa katika sakata la mauaji ya Jamal Khashoggi  kwa ushirikaino na uongozi wa  rais Trump.

Jarida hilo limezungumza kuhusu washukiwa 17 kuhusu sakata hilo ambao walipewa amri kutoka ngazi za juu bila ya kuhoji  wahusika hao wa ngazi za juu.Habari Zinazohusiana