Aina tatu za lugha: Maandamano, Upinzani na Utawala

Ufafanuzi kutoka kwa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt

Aina tatu za lugha: Maandamano, Upinzani na Utawala

Zama hizi za utandawazi ambazo tunaishi zinabadili maisha yetu kwa namna nyingi sana. Mabadiliko ambayo yalishindwa kupokelewa na kukubaliwa katika jamii kwa karne, yanapolekewa na kukubaliwa kwa muda mfupi. Mwanasaikolojia David Harvey hali hii ameifafanua kama “Msongamano wa muda na mahali”.

Katika zama hizi matukio, mahusiano na mabadiliko yamekuwa yakitokea kwa kasi inayochanganya kichwa cha binadamu. Jamii zinazotoka Jiografia zilizombali zinashabihiana wakati zile za Jiografia ya karibu zinakinzana. Vitu ambavyo havikufahamika hapo mwanzo sasa hivi vinafahamika na vile ambavyo vilifahamika kwa uraisi sasa hivi vimekuwa katika hali ya kutofahamika tena.

Kama vile alivyofafanua Ortega Gasset “ Ustaarabu wa kiwango cha juu husababisha tatizo korofi. Na kadiri zinavyopigwa hatua kuelekea kwenye maendeleo ndivyo aina ya hatari inayowakabili pia huongezeka. Kila siku zinavyozidi kwenda ndivyo maisha yanavyozidi kuwa mazuri zaidi lakini hili linakuja na aina ya matokeo ambayo hayakwepeki maisha yanakuwa tata zaidi, magumu zaidi”.

Tunakuletea ufafanuzi wa mada hii uliofanywa na Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL, mkuu wa kitivo  cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt...

Tunachotaka kuelezea ni jinsi gana jamii zenye utambulisho tofauti,tamaduni tofauti, miundo tofauti, asasi tofauti zinaweza kuwasiliana kwa kutumia lugha na kuelewana.Kwa sababu unapopotea uhusiano wa asili maisha  huwa katika hali tete sana.Watu wa utambulisho tofauti tofauti wanapokutana pamoja huleta hali ya wasiwasi na mashaka.

Moja ya sababu ya kubaguana, kutengana, kuchukiana  kunatokana na hii hali ya wasiwasi na msahaka.Hata katika kipindi cha kawaida Lugha inayotumiwa huwa ni muhimu kuzingatiwa.

Lakini katika hali ya wasiwasi na mashaka aina lugha, tabia na misimamo inayotumika katika mawasiliano dhidi ya makundi, mashirika, serikali na watu wengine ni muhimu sana katika kujenga  mahusiano yenye tija baina ya wahusika. Katika hali ya kawaida au hali ya ufahamu tabia nyingi ambazo zinakukubalika  ni nzuri, zinapotumika wakati wa mashaka na wasiwasi huweza kuzua mtafuruku wa hali ya juu.

Ni aina gani ya Lugha/Maelezo/Misimamo: Maandamano,Upinzani,Utawala ?

Kama watu binafsi, makundi, asasi, au nchi tutumie lugha ya aina gani kuwasiliana na watu tunaotofautiana nao  au tunaofanana  tunaoishi nao sehemu moja ?  Majibu ya swali hili mara nyingine humaanisha kukubaliana na tabia tusizozikubali.

Katika makala hii tutajaribu kulijibu swali hilo kwa mtazamo wa mtu binafsi. Ingawa taswura itayowekwa inaweza kutumika kulijibu swali hili kwa ngazi ya makundi, jamii na hata baina ya serikali.

Katika mahusiano baina ya watu je inabidi watu hao wawe na misimamo ya aina  gani ? Je mara zote watumie lugha ya kujibizana ?  Je watumie lugha ya kupingana “ Bw mpinzani” au watumie lugha iliyojengwa kwa misingi ya kukuza mahusiano, lugha ya kiutawala ?

Ngoja nielezee  ninachomaanisha kwa kutumia mfano wa mkutano mmoja nilioshiriki. Nilialikwa kwenye mkutano wa mawaziri na wabunge wa nchi za kiislamu. Mkutano huo ulifanyika kwenye hoteli na walioruhusiwa kushiriki ni waalikwa tu.

Kila mzungumzaji alikuwa   anatumia maneno ya kiarabu ya kujiapiza “Wallahi, watallahi, wabillahi” kutoa hotuba ya kusisimua. Ukumbi ulirindima kwa vigelele na misemo mbalimbali iliyosemwa siku hiyo.

Ilipofika zamu yangu kuzungumza nilisema maneno haya “Ndio katika dunia ya  waislamu kuna matatizo makubwa , kuna maumivu makubwa lakini huu ni mkutano binafsi. Matatizo haya inabidi tuyatafutie ufumbuzi kwa utulivu” Kama unavyoweza kudhani mkutano ambao ulikuwa umejaa jazba alafu anatokea mtu  anaitisha utulivu.

Ndivyo ilivyokuwa katika mkutano ule mimi ndio nilipigiwa makofi na kushangiliwa kidogo. Pamoja na yote hayo katika mkutano ule nilipata nafasi ya  kufundisha aina tatu za lugha za kuzungumza na aina tatu za misimamo.

 Mosi Lugha ya mtaa au lugha ya maandamano. Lugha ya mtaa huhitajika kutumika mara kwa mara na inapotumika panapohitjaika huwa ni lugha yenye ufanisi  sana.Mara nyingine kufanya mikusanyiko, maandamano na upinzani ndio huwa njia fanisi ya kutatua tatizo na kufikia malengo, Kama jinsi ilivyotokea Julai 15.

Mara nyingine ujumbe au msimamo ambao hauwezi kufikishwa kwa njia ya  aina yeyote ile isipokuwa kufikishwa kwa lugha ya mtaa (maandamano). Lakini tuseme kwamba lugha ya mtaa inapohitajika na ikatumika ipasavyo huwa na ufanisi. Kitu ambacho hakiwezekani ni kutumia lugha ya mtaa mara zote.Lugha ya mtaa haiwezi kujenga utamaduni imara ulio tajiri. Lugha iliyokuwa ikitumiwa katika mkutano binafsi niliokuwa nauzungumzia ni lugha ya mtaa( lugha ya kimaandamano)

Pili lugha ya Upinzani. Lugha ya upinzani ni kuwa ndani ya mfumo bila kuwa na malengo ya kujenga au kufikia kitu chochote isipokuwa inapinga kitu chochote au msimamo wowote utaoonyeshwa au kuletwa na utawala. 

Katika mahusiano ya marafiki, au wafanyakazi wa shirika wenye lugha ya upinzani mara zote wao ni kulalamika tu.Vyama vya siasa ambavyo hupinga bila kutoa suluhisho ni mfano wa lugha hii.

Lugha ya upinzani inapokuwa ni lugha pekee inayotumika hupinga kila kitu kuanzia kupinga yasiyofaa mpaka kufikia kupinga yale yanayofaa. Lugha ya upinzani inapotumika ikatoa pia na njia mbadala ya kutatua tatizo basi huweza kuleta maendeleo.

Tatu ni Lugha ya utawala . Ni lugha/maelezo/msimamo inayobembeleza, inayojenga na inayoasisi. Msimamo huu sio tu ule wa utawala wa kisiasa bali hata kwa watu binafsi.

Baadhi ya watu hujenga mahusiano kwa kutumia lugha ya maandamao, wengine hujenga mahusiano kwa kutumia lugha ya upinzani wakati wengine hutumia lugha ya kiutawala katika harakati za kuendana na mazingira

Vijana mara nyingi lugha yao huwa ya majibizano, lugha ya kiupinzani kwa sababu ujana ni maji ya moto. Lakini kadiri miaka inavyoongezeka au wadhifa unapopanda basi lugha hubadilika na kuwa lugha ya kiutawala zaidi. Kwa muda fikiria msemo usemao “Anayevaa taji uzito wake humuelemea” Kama umefikia umri mkubwa, au umefikia cheo fulani kikubwa lakini bado katika mahusiano yako na watu unatumia lugha za kichochezi, au unafanya upinzani usiokuwa na faida basi utakuwa mtu wa ajabu au Mpinzani wa kudumu. Mtu anapofikia cheo au umri fulani anategemewa awe mtulivu na mwenye kutatua matatizo bila papara na kwa uangalifu.

Lugha zinazotumiwa dhidi ya wengine inabidi iwe ni lugha inayojenga .

Kwa watu, jamii, asasi, mataifa wanaotumia lugha hii mara zote huwa na faida. Mahusiano baina ya watu na misimamo yao huathiriwa moja kwa moja kwa na aina ya lugha wanazotumia.

Nje ya lugha hizi tatu, kuna aina ya ushawishi ambao hutumiwa kwa ajili ya kujipatia manufaa fulani ambayo tunaweza kuuita lugha ya kiushawishi.Lakini vile  haizalishi kitu chochote inabidi isionekane kama ni  lugha.

Ukilinganisha lugha ya maandamano,lugha ya Upinzani na ile ya kiutawala. Lugha ya kiutawla inahitaji aina fulani ya ukomavu na uzoefu. Kuweza kuitumia lugha ya kiutawala inahitajika pia mchakato maalum.

Lugha ya kiutawala ni lugha ambayo watu hujifunza kutokana na makosa na lugha ambayo pia huweza kuendelezwa kupitia makosa

Je wewe katika maisha yako ya kila siku, mar nyingi unajiona ni mtu wa misimamo gani, ni aina gani ya lugha unayoitumia ?.

Ufafanuzi kutoka kwaProf. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt.Habari Zinazohusiana