Mkanyagano katika klabu ya usiku wasababisha vifo vya watu 6 nchini Italia

Mkanyagano uliotokea kwenye klabu ya usiku nchini Italia umesababisha vifo vya watu 6 na wengine wengi kujeruhiwa.

Mkanyagano katika klabu ya usiku wasababisha vifo vya watu 6 nchini Italia

 

Watu 6 wamefariki baada ya kutokea mkanyagano katika klabu ya usiku pembezoni mwa pwani ya Adriyatic mjini Corinaldo nchini Italia. 

Katika taarifa iliyotolewa na kamanda wa polisi wa Ancona ilisema mkanyagano uliotokea katika klabu ya usiku inayojulikana kwa jina la Lanterna Azzurra  mjini Corinaldo umesababisha vifo vya watu 6, na watu wengine 50 kujeruhiwa. 

Baadhi ya watu miongoni mwa majeruhi hali zao ni mbaya.

Sababu iliyosababisha mkanyagano huo haikuwekwa wazi. Uchunguzi kuhusiana na mkanyagano huo unaendelea imefahamishwa.

 Habari Zinazohusiana