Rais Erdoğan na maandamano nchini Ufaransa

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan azungumzia maandamano yanayoendelea nchini Ufaransa

protesto Paris.jpg
Bélgica.jpg

Rais wa Uturuki  Recep Tayyıp Erdoğan  azungumzia  maandamano  yanayoendelea nchini Ufaransa.

 Rais wa  Uturuki  azungumzia maandamano yanayoendelea nchini Ufaransa  kwa muda wa wiki  zaidi ya mbili.

 Rais Erdoğan amesema kuwa  picha kuhusu maandamano zinazooneshwa katika vyombo vya habari   zinaonesha kuwa Magharibi  tayari imeshindwa  kuheshimu misingi ya demokrasia na haki za binadamu.

Maandamano  yameripotiwa katika maeneo tofauti barani Ulaya ikiwe mjini Paris.

Uturuki inakemea uharibifu  unasababishwa na  waandamanaji wasiokuwa na nidhamu na kukemea pia mwenendo wa askar iwa kutuliza ghasia wanavyokabiliana na waandamanaji kwa kuwashambulia .

Maandamano ya kupinga  kupanda bei za mafuta nchini Ufaransa yalianza  Novemba 17  yamekuwa maandamano  yenye waandamanaji  wenye jazba nchini Ufaransa.

Vuguvugu la waa ndamanaji waliovalia sare za  manjano limevuka mipaka  hadi  nchini Ubelgiji na Uholanzi.

Waandamanaji wadai kupunguzwa na bei za mafuta na kupinga ukhali wa maisha kila  kukicha nchini Ufaransa.

Waziri  mkuu wa  Ufaransa alesema kuwa idadi ya askari wa kukabiliana na waandamanaji itaongezwa kote nchini Ufaransa kuzuia  waandamanaji  wenye nia mbaya na taifa.Habari Zinazohusiana