Rais wa zamani wa Armenia akamatwa

Mahakama nchini Armenia imeamuru rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Kocharian kukamatwa kwa kosa la kuvunja katiba

Rais wa zamani wa Armenia akamatwa

 

Mahakama nchini Armenia imetoa amri ya kukamatwa rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Kocharyan, kwa kuhisishwa na vifo vya watu 10 vilivyotokea nchini humo mwaka 2008 wakati wa maandamano.

Idara ya upelelezi  binafsi nchini Armenia ilifungua mashtaka mahakamani dhidi ya rais huyo wa zamani ikimshutumu kwa kuvunja katiba ya nchi hio. Kocharyan alikuwa rais wa taifa hilo kati ya mwak 1998 mpaka mwaka 2008.

Kocharyan ameyakana mashtaka hayo kwa kujitetea kwamba kulikuwa kuna shinikizo la kisiasa.

Mwezi Julai mahakama kuu ya Yereven ilitoa amri ya kukamatwa kwa Kocharyan kwa kosa la kuvunja katiba. Kocharian aliachiwa kwa dhamana

Maandamano yaliandaliwa  kupinga uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2008 nchini Armenia . Katika maandamano hayo yaliyofanyika Machi 1, 2008 polisi 2 na raia 10 walipoteza maisha. 

 


Tagi: Armenia

Habari Zinazohusiana