Spika wa bunge la Uturuki na mwenzake wa bunge la Iran wafanya mazungumzo

Spika wa bunge la Uturuki Binali Yıldırım kwa sasa yupo mjini Tehran kuhudhuria mkutano wa wasemaji wa bunge katika kujadili suala zima la ugaidi na uchochezi.

Spika wa bunge la Uturuki na mwenzake wa bunge la Iran wafanya mazungumzo

Spika wa bunge la Uturuki Binali Yıldırım kwa sasa yupo mjini Tehran kuhudhuria mkutano wa wasemaji wa bunge katika kujadili suala zima la ugaidi na uchochezi.

Kabla ya kuanza kwa  mkutano huo,spika wa bunge la Uturuki amesema kuwa Uturuki na Iran ni nchi ambazo zimekuwa na uhusiano mzuri kwa karne nyingi.

"Sisi ni kama ndugu.Tatizo la Iran ni tatizo la Uturuki.Furaha ya Iran ni furaha ya Uturuki",alisema Yıldırım.

Msemaji huyo vilevile amelaani shambulizi lililotokea kusinimashariki mwa mji wa Chahabar nchini Iran na kusababisha vifo vya takriban watu wawili huku wengine 27 wakiwa wamejeruhiwa.Yildirim ametuma salamu za rambirambi kwa wote waliofikiwa na janga hilo.

Msemaji wa bunge la Iran,Larijani kwa upande wake amemshukuru Yildirim kwa kukubali mwaliko wake na kuzungumzia kuhusu mafanikio ya mkutano wa 11 wa APA uliofanyika kati ya 28 Novemba na 3  Desemba mjini Istanbul.

Larijani amesema kuwa mkutano huo uliwapa fursa ya kuzungumza masuala mbalimbali ya kanda.

Akikumbushia wakati Binali Yıldırım alikuwa bado waziri mkuu wa Uturuki,Larijani amezungumzia uhusiano mzuri ulioimarishwa kati ya Iran na Uturuki.

Kiongozi huyo wa bunge la Uturuki atatoa hotuba kuhusu ugaidi na uchochezi katika mkutano huo wa wasemaji wa bunge la Iran,Urusi,China,Pakistan,Afghanistan na rais wa Iran Hassan Rouhani.

 

 Habari Zinazohusiana