Trump amshambulia Rex Tillerson

Rais wa Marekani Donald Trump ameutumia  ukurasa wake wa Twitter kumshambulia aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Rex Tiilerson.

Trump amshambulia Rex  Tillerson

Rais wa Marekani Donald Trump ameutumia  ukurasa wake wa Twitter kumshambulia aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Rex Tiilerson.

Hio ni baada ya Tillerson kusema kuwa Trump alikuwa akimlazimisha kufanya vitu kinyume na sheria.

Trump amemwagia sifa waziri wa mambo ya nje wa sasa wa nchi hiyo Mike Pompeo na kuendelea kwa kusema kuwa Tillerson alikuwa hana sifa kamili na wala hakuleta mafanikio wakati alipoutumikia wadhifa wake.

"Mike Pompeo anafanya kazi nzuri sana na ninajivunia kuwa na waziri kama yeye.Mwenzake Rex Tillerson hakuwa na akili za kutosha kufanya kazi yake.Alikuwa mjinga kupita kiasi na nilitakiwa kumfukuza kazi mapema iwezekanavyo.Alikuwa ni mvivu kupita maelezo.Kwa sasa tunatizama mambo mapya kwa ajili ya taifa letu.",Trump aliandika katika ukurasa wake wa Twitter.

Ujumbe huo wa Twitter umekuja siku moja baada ya Rex Tillerson kutangaza wakati akiwa Houston kuwa Trump mara nyingi alikuwa akimwambia afanye vitu ambavyo vilikuwa vinaivunja sheria.

"Alikuwa akiniambia nataka kufanya hivi ama nataka kufanya vile.Nilikuwa nikimjibu na kumwambia kuwa ' Mheshimiwa rais nimekuelewa unachotaka kufanya lakini huwezi  kufanya kwa njia hiyo kwani ni kinyume na sheria",Tillerson alisema  kulingana na video iliyorekodiwa na kituo cha habari cha CBS.

Tillerson aliendelea kwa  kusema kuwa Trump ni mtu asiyekuwa na heshima,hapendi kusoma,hasomi ripoti za kumjuza yanayoendelea na kwamba Trump huchukua maamuzi jinsi anavyojiskia.

Rex Tillerson,waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Marekani alifutwa kazi na Trump miezi 14 iliyopita .

Bwana Tillerson amesisitiza kuwa alikuwa hamfahamu Trump mpaka siku alipochaguliwa.

Rex Tillerson vilevile anaamini kuwa mtandao wa Twitter umewafanya wamarekani wengi kutokuwa makini katika kufuatilia mambo yanayoendelea katika taifa lao.

 Habari Zinazohusiana