Watu zaidi ya 700 wakamatwa katika maandamano nchini Ufaransa

Jeshi la Polisi lawakamata waandmanaji zaidi ya 700 katika maandamano Jumamosi ya kupinga kupanda kwa bei za mafuta

Watu zaidi ya 700 wakamatwa katika maandamano nchini Ufaransa

Jeshi la Polisi lawakamata waandmanaji zaidi ya 700 katika maandamano Jumamosi ya kupinga kupanda kwa bei za mafuta

Waandamanaji kwa mara nyingine walimiminika  mjini Paris  kushiriki katika maandamano ya kupinga kupanda kwa bei za mafuta.

Ikiwa ni wiki ya nne, waandamanaji wakiandamana nchini Ufaransa. Katika maandamano hayo watu zaidi ya 700 wamekamatwa katika maandamano ya Jumamosi ambayo yalikuwa yakihofiwa kuwa na ghasia ambazo zingesababisha uharibifu mkubwa.

Zaidi ya askari  90 000 walipelekwa katika   barabara ilio karibu na Champs-Elysees kwa ajili ya kukabiliana na waandamanaji.

Waziri wa mambo ya ndani Christophe Castaner  na msaidizi wake wamewaambia waandishi wa habari  kuwa watu waliokamatwa  wamewekwa rumande.

Kwa upande mwingine  waziri mkuu wa Ufaransa  ametoa shukrani kwa viongozi wa kisiasa, viongozi wa makundi ya kutete maslahi ya wafanyakazi  na waandamanaji walioonesha uoleo baada ya kutolewa wito wa kusitisha maandamano badala ya kushirikiana na waandamanaji ambao  malengo yao yalikuwa  uharibifu wa mali.Habari Zinazohusiana