Çavuşoğlu : "Uturuki haiombi ushauri katika harakati zake za kupambana na ugaidi"

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki asema kwamba Uturuki haiombi ruhusa kwa yeyote yule katika harakati zake za kupambana na ugaidi

Çavuşoğlu : "Uturuki haiombi  ushauri  katika harakati zake za kupambana na ugaidi"

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki asema kwamba Uturuki haiombi ruhusa kwa yeyote yule katika harakati zake za kupambana na ugaidi.

Mevlüt Çavuşoğlu  asema kuwa Uuruki haiombi ruhusa kwa yeyote yule katika harakati zake za kupambana na ugaidi na kusema kuwa , Marekani  ilichukuwa uamuzi wa kuondoa wanajeshi wake nchini Syria kutokana na  uamuzi wa rais Erdoğan kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amesema kuwa  uamuzi wa rais Erdoğan  wa kupambana na magaidi na kuwaangamiza ni moja ya sababu zilizopelekea Marekani kutangaza kuwaondoa wanajeshi wake nchini Syria.

Rais Erdoğan alichukuwa uamuzi  kuondoa vitisho vya ugaidi katika mipaka ya Uturuki.

Katika mkutano uliofanyika mkoani Antalya, Mevlüt Çavuşoğlu  amethibitisha kuwa Uturuki taifa pekee ambalo  limekabiliana  kwa wakati mmoja na makundi tofauti ya kigaidi yanayotishia usalama wa Uturuki na kutafuta suluhu na utulivu nchini Syria.

Uturuki imedhamiria kukabiliana na magaidi  Mashariki mwa Frati.Habari Zinazohusiana