Bunge la Irak laomba ufafanuzi baada ya tume kutoka nchini humo kufanya ziara Israel

Bunge la Irak laomba ufafanuzi baada ya tume kutoka nchini humo kufanya ziara Israel

Bunge la Irak laomba  ufafanuzi baada ya tume kutoka nchini humo  kufanya ziara Israel

Bunge la Irak laomba ufafanuzi baada ya fununua kuwa tume kutoka Irak imefanya ziara  Israel.

Kulingana na taarifa ambazo zimetolewa vya vyanzo vya habari nchini Irak,  waziri mkuu wa Irak  ametoa ujumbe  katika  kurusa zake  katika mitandoa ya kijamii  tume kutoka Irak  huenda ilifanya ziara  Israel.

Waziri mkuu wa Irak anatakiwa  kujibu tuhuma hizo  bungeni  kuhusu ziara  hiyo mwaka 2018.

Mbunge wa chama cha Dawa kinachoongozwa na Nuri al Maliki, Aliya Nesif amesema amekwishakusanya saini  7 za wabunge  kwa lengo la kuendesha  uchunguzi  kuhusu  tuhuma hizo  kuhusu ziara  hiyo Israel mwaka 2018.

Nesif amesema kuna umuhimu wa kuendesha uchunguzi kuhusu suala hilo.

Tume hiyo ilikuwa ikijumuisha wawakilishi wa madhehebu ya shia na suni.

Tuhuma hizo  zinamtaja  mbunge Khaled al Mafraji na Ahmed Djerba walikuwa katika ziara hiyo.

Wabunge hao wametupilia mbali tuhuma hizo.


Tagi: Israel , Irak

Habari Zinazohusiana