Kuambatanisha magaidi wa PKK na jamii ya wakurdi ni kosa lisilokubalika

Kuambatanisha magaidi wa PKK na jamii ya wakurdi ni kosa lisilokubalika asema  Ibrahim Kalın msemaji wa ikulu Ankara

Kuambatanisha magaidi wa PKK na jamii ya wakurdi ni kosa lisilokubalika

Kuambatanisha magaidi wa PKK na jamii na wakurdi ni kosa lisilokubalika asema  Ibrahim Kalın msemaji wa ikulu Ankara.

Msemaji wa ikulu  mjini Ankara Ibrahim  Kalın  amekemea vikali  kauli za rais wa Marekkani Donald Trum kuhusu Uturuki.

Ibrahim Kalın amesema kuwa  Marekani na rais wake Donald Trump  hauwezi kuwa  mshirika wa kundi la kigaidi   bali mshirika wa kimkakati wa ambae anatakiwa kukemea ugaidi.

Msemaji wa ikulu Ibrahim amemjibu rais wa Marekani  kupitia ujumbe wake aliotoa katika  ukurasa wake wa Twitter.

Katika ujumbe wake huo, Ibrahim amemfahamisha rais Trump kuwa  ni kosa kubwa kuambatanisha  wanamgambo wa kundi la PKK  na jamii ya wakurdi. Kundi la PKK na  tawi lake la YPG ni makundi ya kigaidi  ambayo yanafahamika katika ukanda.

Uturuki inapambana na  ugaidi  sio na jamii ya wakurdi alisema Ibrahim Kalın katika uumbe wake na kusema kuwa ni wajibu  kwa Uturuki  kuwalinda wakurdi na wasyria wengine dhidi ya ugaidi.

Rais Trump katika ujumbe wake katika ukurasa wake Twitter alisema kuwa Marekani imeanza kuwaondoa wanajeshi wake Syria na mapambano dhidi ya kundi la wanamgambo wa Daesh yataendelea.

Katika ujumbe wake huo Trump alitoa vitisho  dhidi ya Uturuki  iwapo wanamgambo wa PKK/YPG watashambuliwa  kabla ya kuwekwa eneo salama la mili 20 mpakani mwa Uturuki na Syria.Habari Zinazohusiana