Mazungumzo kati ya Trump na Erdoğan

"Uturuki haina tatizo na Wakurdi na inalenga kupambana na makundi ya ugaidi yanayotishia usalama wa taifa", Rais Recep Tayyip Erdoğan amesema katika mazungumzo yake na rais wa Marekani Donald Trump.

Taarifa kutoka ikulu ya urais wa Uturuki imesema kuwa rais Erdoğan na mwenzake wa Marekani Donald Trump wamezungumza kuhusu hali ya usalama katika ukanda kaskazini mwa Syria.
 
"Uturuki inaunga mkono uamuzi wa Trump juu ya uondoaji wa vikosi vya Marekani kutoka Syria", Erdogan alisema, akiongeza kuwa Uturuki itatoa kila aina ya msaada katika suala hilo.

Viongozi wawili wamekubaliana kuendeleza uhusiano wa kiuchumi wa nchi mbili.
 
Mazungumzo hayo yamekuja baada ya Trump kuandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa Marekani itauharibu uchumi wa Uturuki endapo nchi hiyo itawapiga wakurdi,ikishindwa kutofautisha wakurdi na magaidi wa PKK.

Habari Zinazohusiana