Saudia yakana kuwa na mpango wa kufungua ubalozi Damascus

Saudi Arabia imekanusha ripoti kwamba imepanga kufungua ubalozi wake katika mji mkuu wa Syria wa Damascus.

Saudia yakana kuwa na mpango wa kufungua ubalozi Damascus

Saudi Arabia imekanusha ripoti kwamba imepanga kufungua ubalozi wake katika mji mkuu wa Syria wa Damascus.

Baadhi ya tovuti za habari zimekuwa zikisema kuwa waziri wa mambo ya nje wa Saudi Ibrahim al-Assaf ametangaza kuwa Riyadh ilipendekeza kufungus tena ubalozi wake wa Damascus siku ya Alhamisi.

"Taarifa hizi haziko sahihi," Wizara ya Nje ya Saudi imesema katika taarifa yake siku ya Jumatatu.

Mwezi uliopita UAE na Bahrain, nchi ambazo ziliunga mkono upinzani nchini Syria - zilitangaza mpango wa kufungua balozi zao huko Damascus baada ya miaka saba.

Syria imekuwa katika mgogoro na mapigano toka mwaka 2011.

Maelfu ya wananchi,hasa wanawake na watoto wamepoteza maisha katika mapigano hayo.Habari Zinazohusiana