Je ndio mwisho wa maadili ?

Sehemu ya pili ya ufafanuzi, umetolewa na mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL

Je ndio mwisho wa maadili ?

Wiki iliyopita katika makala hii tulionyesha ni jinsi gani mmomonyko wa maadili umefikia kiwango cha juu. Tunaishi katika kipindi ambacho kanuni, wema, kusaidiana, fadhila, haki na maadili mengine ya namna hiyo yamesahaulika. Tulisema kwamba jina linalofaa kuziita  zama hizi ni zama za mwisho wa maadili (the end of values). Tulisema kwamba kwa jicho la ndege  dunia ikitazamwa kutoka juu ingeonekana ni kiasi gani mmomonyoko wa maadili ulivyozitafuna jamii.

Tulimalizia kwa kutazama athari za mmomonyoka wa maadili  kwa  Umoja wa Mataifa na Umoja wa Ulaya.  Tuendelee..

Mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL anafafanua...

Marekani

Siku sio nyingi sana, mpaka jana Marekani ilikuwa ikikumbukwa kama nchi ya  “Ndoto ya Amerika”  (american dream). “Mtindo wa  maisha ya kiamerika” (American way of life) karibu katika kila nchi ulikuwa  ndio mtindo wa kisasa. Leo hii kama ukifanyika utafiti wa maoni ya umma kuhusiana na Marekani inavyochukuliwa, karibu katika nchi zote matokeo yatakuwa ni mtazamo hasi kupata kutokea katika historia ya taifa hilo.

Leo hii kuna wahamiaji 6000 ( takwimu za maandishi)  kutoka Amerika ya kusini peke yake katika mipaka ya Marekani wakisubiri kuingia nchini humo . Nchi kama Uturuki, Lebanon, Jordan mara nyingine kwa usiku mmoja tu hupokea wahamiaji wengi zaidi ya hao. Sasa Nchi namba moja duniani hivi sasa ndio inayoongoza kwa kuwa na wahamiaji wengi wanaosubirishwa mipakani. Mbaya zaidi moja ya nchi tajiri duniani badala ya kuja na suluhisho kama lile la Ulaya la kuuvunja ukuta wa Berlin, inatumia jeshi na kufikiria kusimamisha kuta dhidi ya wahamiaji. Haya yanayofanyika na yatayofanyika  yumkini gharama yake ni kubwa zaidi ukilinganisha na gharama ya kutatua matatizo ya wahamiaji.

Uongozi wa sasa wa Marekani bila kuzingatia uhalali  wa jambo umekuwa ukitazama maslahi yake tu. “Marekani kwanza”, “Ifanye Marekani taifa kubwa tena” ni baadhi ya kauli mbiu za uongozi uliopo madarakani hivi sasa nchini  Marekani. Inawezekana Marekani hivi sasa inafikiria kujitoa kwenye mikataba yote , Tumeona imejitoa kwenye mkataba wa kuzuia ongezeko la joto duniani “Makubaliano ya hali ya hewa ya Paris”, tumeona imejitoa kutoka shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO). Maamuzi yote hayo ya Marekani yamekuwa yakileta wasiwasi dunia nzima.

Mara ya mwisho rais wa Marekani Donald Trump katika mkutano wa mwisho wa baraza la uongozi la Umoja wa mataifa alisema Marekani haikubaliani na “Idiolojia ya Utandawazi”. Kauli hii ya mheshiwa Trump sio zamani sana, miaka kadhaa iliopita ilikuwa ni kauli inayoweza kutolewa na kiongozi mmoja wa dunia ya tatu.Kauli kama hio kutolewa na kiongozi mkuu wa Marekani ni suala ambalo hata katika ndoto haikuweza kufikirika.

 Leo hii Marekani nayo kama vile  mataifa mengine ya magharibi yanaonekana tu kuhubiri na kutetea demokrasi, uhuru, haki za binadamu na maadili mengine ya aina hiyo ilhali kiuhalisia matendo yao yapo mbali na maneno yao. Sio tofauti na ilivyokuwa katika historia ya ustaarabu wa magharibi pale walipo tafasiri tofauti aya za Injili  walipoona aya hizo zinaenda kinyume na maslahi yao.

China-Urusi

China na Urusi sio miongoni mwa nchi ambazo katika karne hii ya mwisho zimekuwa zikifafanua maadili na daraja zake. Pamoja na hayo China ni moja ya nchi ambayo imekuwa  ikiendelea kwa kasi kubwa. Nchi zote hizi mbili zina nguvu katika siasa za dunia. Ni nchi ambazo zinakura turufu  “VETO” katika baraza la usalama la umoja wa mataifa. Kwa kuwa mataifa yote haya mawili hayako wazi vya kutosha, Jumuiya ya kimataifa haifahamu vizuri sera za ndani za mataifa haya . Hatua za Putin dhidi ya wapinzani wake wa kisiasa zinapingwa kwa kiasi kikubwa. Kwa upande wa China nayo kinachosemwa na vyombo vya kimataifa kama uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu mashariki mwa Turkistan haifahamiki  habari hizo zina ukweli kiasi gani kwa kuwa taifa hilo nalo sera zake haziko wazi.

Dunia ya Waislamu

Katika  karne za hivi karibuni mataifa ya kiislamu nayo sio katika mataifa yanayo fafanua maadili na daraja zake kwa ngazi ya kidunia. Mengi yao ni mataifa ya kifalme au yenye kufuata sharia au kanuni zisizo za kidini. Vyovyote vile utakavyoamua kuzifafanua aina ya siasa katika mataifa ya kiislamu, mataifa haya nayo yamekuwa yakifuata tawala za kiimla, au kidemokrasia.

Hasa hasa unapotazama mashariki ya kati Watawala hawajali kama wanaowatawala wanawaridhia au la . Watawala wanajali zaidi maslahi ya wadau wakubwa wa kidunia ambao mara nyingi ndio wanakuwa wamewafadhili kuingia madarakani. Wadau hao wakuibwa wa kidunia nao bila kupepesa macho huweza kuwakumbusha watawala hawa juu ya hili. Hata kama mataifa haya yangekuwa ya kiwajibikaji, hali ilivyo hivi sasa, baadhi ya mataifa haya yanapitia kipindi kibaya kabisa cha maumivu kupata kutokea katika historia ya mataifa hayo. Wanajamii wa mataifa haya wapo katika juhudi za kuyakimbia kuokoa maisha yao.

Mengi ya mataifa haya ya mashariki ya kati Watawala wapo katika juhudi ya kutengeza maadili ambayo yatawawezesha  walinde madaraka yao milele.

Mwisho wa akili za Waangazishaji: Toka Frankshtain mpaka akili bandia

Mwandishi mmoja mwanamama wa kiingereza Mary Shelley, akiwa na umri wa miaka 19  tu mnamo mwaka 1818 aliandika  kazi yake “Frankenstein”. Kazi hii ni zaidi ya kitabu cha tamthilia unaweza kuona akili za mwandishi wa kitabu hiki ni ambayo ipo mbali kabisa na utamaduni, dini, na taasisi nyingine ni aina ya akili ya kiuangazishaji, kiulemishaji, kisekulari, chanya na iliyojengeka katika misingi ya fikra huru na halisi. Leo hii akili za kiuangazishaji zimejishughulisha na kutengeneza akili bandia (kutengeneza binadamu). Akili za kiuangazishaji ambazo hazikutambua mipaka ndizo zilizopelekea vita kuu ya kwanza na ya pili ya dunia. Katika vita hivi itakumbukwa ni kwa kiasi gani sayari yetu na utu wetu ulivyopitia majaribu makubwa. Kila mtu ni shahidi wa janga hilo.

Binadamu ambaye hana maadili wala hisia zozote isipokuwa mwenye nguvu za kimakenika na uwezo wa kuleta maendeleo mwenye nguvu zaidi ya binadamu wa kibaiolojia na mwenye uwezo wa kumuongoza binadamu wa kibaiolojia,Binadamu mwenye akili za bandia, Dunia inaenda wapi katika mazingira kama haya ?.Inaonekana kana kwamba mwisho wa binadamu utaletwa na binadamu mwenyewe.

Binadamu mwenye kuendekeza Anasa   

Uangazishaji, Usekulalishaji,maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, pamoja na kupoteza matumaini kwenye dini, taasisi na idilolojia vimechangia  kadiri siku zinavyokwenda binadamu wawe wenye kuendekeza anasa na kuponda raha. Hili linaonekana zaidi kwa vijana. Kadri siku zinavyokwenda ndivyo idadi ya watu ambao lengo lao kuu ni kuponda raha na kula bata inavyoongezeka.

Watu hawa aina ya mahusiano wanayoyajenga na familia zao, marafiki zao, shule, mazingira, maeneo ya kazi, hali nchi, wanyama  na viumbe wengine huyajenga kwa kuzingatia kigezo cha kupata raha “kula bata”. Aina ya watu wa namna hii ndio wamesababisha tatizo linalotukabili kuwa kubwa siku hadi siku. Unapobadilika na kuwa mtu usiye na maadili lengo lako kubwa ni kula bata tu kwa hakika unaupoteza utu na unakuwa si mtu tena.

Kwa kuzingatia tulichoelezea inaweza kusemwa kwamba mmomonyoko wa maadili unaweza kuzungumzwa katika ngazi ya muundo wa taasisi kama vile serikali. Inaweeza kusemwa kwamba watu binafsi na makundi ya kiutambulishi na idiolojia kubwa ambazo haziko chini ya serikali na mashirika makubwa ya kimataifa wameendelea kuwa na maadili pamoja ukinzani wote tulioutaja.  

 

Ndio watu wasiofungamana na taasisi wanaweza kuwa ndio watetezi na waendelezaji wa maadili.Tunaweza kupata matumaini  zaidi ya utatuzi wa  changamoto ya maadili kutoka kwa miundo isiyokuwa ya kitaasisi. Pamoja na yote hayo kwa kujua kwamba dunia ipo kimuundo wa kitaasisi zaidi matumaini yetu ya utatuzi wa changamoto hii kutoka kwa miundo isiyo ya kitaasisi yanapungua.

 

Familia ya binadamu kwa ujumla wake inapaswa kuchukua hatua stahiki katika kusimamisha mchakato huu utaopelekea “mwisho wa maadili”. Na kama kwa umoja wetu tutashindwa kupata suluhisho basi tujiandae kwani mwisho wa kusikitisha wa zama unakaribia kwa kasi.

 

 Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL Mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu chaAnkara Yıldırım Beyazıt.Habari Zinazohusiana