Ndege iliyombeba Sala iliyoripotiwa kupotea yapatikana

Mabaki ya ndege iliyombeba mwanasoka wa Argentina Emiliano Salas yamepatikana

Ndege iliyombeba Sala iliyoripotiwa kupotea yapatikana

Ofisi ya Uingereza ya uchunguzi wa ajali za ndege (AAIB) imefahamisha kwamba mabaki ya ndege iliyombeba mwanasoka wa Argentina Emiliano Sala yamepatikana. Ndege hiyo ilitangazwa kupotea wiki chache zilizopita.

David Mearns wa taasisi ya "Society of Blue water recovery" aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter " Mabaki ya ndege yalipatikana siku ya Jumapili asubuhi".

Ndege hiyo ndogo inasemekana ilipotelea kaskazini mwa visiwa vya Guernsey mnamo siku ya Januari 21.

Sala 28 pamoja na rubani David Ibbotson walikuwa wakitokea Nantes kuelekea Cardiff ambako ndipo makao ya timuCardiff City ambayo Sala alikuwa ametoka kusaini mkataba wa kuichezea wenye thamani ya Euro milioni 17.

Mchezaji huyo inasemekana alikwenda ufaransa kuwaaga wachezaji wenzake wa Nantes FC, timu ambayo alikuwa akiichezea.

 Habari Zinazohusiana