Ubaguzi dhidi ya Waislamu umekuwa kitu cha kawaida nchini Uswizi

Utafiti uliofanywa nchini Uswizi unaonyesha kwamba vitendo vya kıbaguzi dhidi ya Waislamu nchini humo vimekuwa ni jambo la kawaida

Ubaguzi dhidi ya Waislamu umekuwa kitu cha kawaida nchini Uswizi

Mjumbe wa jopo la wakufunzi wa kitivo cha elimu ya historia ya dini chuo kikuu cha Uppsala nchini Uswizi,Prof. Dr. Mattias Gardell, amesema kwamba ubaguzi dhidi ya waislamu nchini Uswızi umekuwa jambo la kawaida. 

Prof. Dr. Gardell ambaye pia ni rais wa kituo cha utafiti cha ubaguzi wa masuala ya tamaduni katika chuo kıkuu cah Uppsala (CEMFOR), alıtoa taarifa ya matokeo ya utafiti ulıofanywa kuhusu uıslamu. Matokeo hayo aliyatangaza katıka televisheni ya taifa hilo (SVT).

Gardell alisema vitendo vya mashambulizi dhidi ya waislamu nchini Uswizi vimeongezeka kwa kiasi kikubwa. Alisema kuna vitendo vipya vya mashambulizı ya kibaguzi dhidi ya waislamu. 'Chuki dhidi ya Uislamu' na cha kushangaza zaidi vitendo hivi vinachukuliwa kama kitu cha kawaida.

Gardell alisema miaka ya hivi karibuni vitendo vya mashambulizi dhidi ya nyumba za ibada pia vimeongezeka kwani mwaka 2018 asilimia 59 ya misikiti nchini Uswizi ilishambulia.

Gardell alisema vyombo vya habari vinachangia kwa kiasi kikubwa vitendo hivyo vya chuki dhıdı ya Uislamu kwani nyingi ya habari wanazozitoa kuhusu Uıslamu ni habari zinazowatia ubaya waislamu.

Gardell alisema kitu chengine cha kushangaza ni kwamba katika maeneo ambayo jamii za waislamu wamekuwa wakiishi, vitendo vya kibaguzi vimepungua.

Gardell alimalizia kwa kusema kwamba anaamini vitendo hivi vya kibaguzi vitakuja kuisha siku moja kwani miaka 100 iliyopita mambo yalıkuwa magumu pia kwa wakristo wakatoliki.

 


Tagi: Uislamu , Uswizi

Habari Zinazohusiana