Umoja wa Ulaya kuijumuisha Saudı Arabia katika orodha nyeusi

Baraza la Umoja wa Ulaya lıpo mbioni kukamisha orodha mpya ya nchi zinazofadhili ugaidi na zilizoshindwa kupambana na utakatısha pesa.

Umoja wa Ulaya kuijumuisha Saudı Arabia katika orodha nyeusi

Umoja wa Ulaya kuijumuisha Saudi Arabia katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi na zilisoshindwa kupambana na utakatishaji pesa.

Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na gazeti la Finacial Times inasema baraza la Umoja wa Ulaya lipo mbioni kukamilisha orodha mpya inayojumuisha nchi zaidi ya 20 ambazo zimeshindwa kukabiliana na utakatishaji pesa.

Kwa mujibu wa habari hio uongozi wa Riyadh hauna mkakati kabambe wa kukabiliana na mikondo ya pesa haramu.

Habari hiyo pıa inaeleza kwamba Ufaransa, Uingereza na Ujerumani wameyapınga maamuzi hayo ya baraza.

Kwa mujıbu wa sheria za umoja wa Ulaya pesa zinazotoka katika mataifa haya hufanyiwa utafiti wa kina zinapofika katika mabenki yaliyo chini ya himaya ya Umoja huo.

 Habari Zinazohusiana