"Waafrika waanza kufunguka macho"

Mabadiliko ya amani na ushirikiano yanaonekana barani Afrika

"Waafrika waanza kufunguka macho"

Mabadiliko ya amani na ushirikiano yanaonekana barani Afrika, amesema mkuu wa Umoja wa Mataifa Jumamosi baada ya kukutana na Moussa Faki Mahamat, mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

"Upepo wa mabadiliko unavuma Afrika, kama ilivyoonyeshwa katika mikataba ya amani kati ya Ethiopia na Eritrea, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati ... na kufanya kazi pamoja na Umoja wa Afrika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Madagascar," alisema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika makao makuu ya Umoja wa Afrika huko Addis Ababa nchini Ethiopia.

Ushirikiano huu una lengo la kuleta  Umoja wa Afrika na kutimiza lengo letu la kuhakikisha mauaji yanasitishwa mpaka kufikia  2020.

 "Ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika ni kiini cha msingi cha kazi ya Umoja wa Mataifa," alisema, pia akitoa ushirikiano wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

 

 


Tagi: dunia , Waafrika

Habari Zinazohusiana