FIFA yaongeza idadi ya nchi zitakazoshiriki kombe la dunia

FIFA yaongeza idadi ya nchi zitakazoshiriki katika kombe la dunia mwaka 2026.

FIFA yaongeza idadi ya nchi zitakazoshiriki kombe la dunia

FIFA yaongeza idadi ya nchi zitakazoshiriki katika kombe la dunia mwaka 2026.

Kwa kawaida nchi thelathini na mbili peke yake ndio huwa zinashiriki mashindano ya kombe la dunia lakini sasa FIFA imeshangaza wengi kwa kuongeza idadi hiyo hadi 48.

Maoni ya wananchi mbalimbali barani Afrika yanaonyesha hii inatazamwa kama fursa kwa nchi nyingi za Afrika kuingia katika mashindano haya.

Hii ni mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kupanuliwa tangu mwaka 1998.

Mpango huu unatarajiwa kufaidisha nchi mbalimbali za Afrika na Asia.

Hata hivyo sio kila mtu amekubaliana na kufurahishwa na maamuzi haya ya FIFA kwani kuna baadhi ya nchi zinadhani uamuzi huu umekuwa ni wa kisiasa zaidi.

 Habari Zinazohusiana