Tunisia yajinyakulia tiketi ya kwenda kombe la dunia la 2018 Urusi

Tunisia yajinyakulia tiketi ya kwenda kombe la dunia la 2018 Urusi baada ya kwenda sare ya kutofungana na Lybia katika mechi ya siku ya 6 na ya mwisho ya michuano ya kufuzu kombe la dunia kwenye kundi A.

Mechi ilifanyika kwenye uwanja wa Radès mjini Tunis ambapo takriban washangiliaji elfu 50 walikuja kuangalia  mechi hiyo akiwemo rais wa Tunisia Béji Caïd Essebsi.

Tunisia imemaliza ikishikilia usikani wa kundi A ikiwa na pointi 13 mbele ya DRC ikiwa na pointi 10. Tunisia ilikuwa inahitaji pointi moja tu ili kujipatia tiketi.

Ni mara ya tano kwa Tunisia au « Aigles de Carthage » kushirika kombe la dunia (1978, 1998, 2002 et 2006). Mwaka 1978 waliandika historia kuwa nchi ya kwanza ya Afrika kupata ushindi walipoifunga Mexico 3-1.

 Habari Zinazohusiana