Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo 

Katika mashindano ya Turkish Airlines open 2017 mjini Antalya Justin Rose ndio amejipatia ushindi.

Mashindano haya yaliyoandaliwa na Turkish Airlines yakiwa ni mashindano ya nane ya Rolex barani Ulaya yamemuwezesha Justin kujipatia ushindi.Nafasi ya pili imechukuliwa na Dyllan Fritelli pamoja na Nicolas Colsaerts.

Kwa upande mwingine katika mashindano hayo timu ya Uingereza imevunja rekodi.Timu hiyo imeweza kupiga mpira wa golf ndani ya sekunde 32.7 na kuvunja rekodi ya dunia.

Rekodi zilizopitwa zilivunjwa na Ufaransa 34.87 na Afrika kusini 32.9.

 

Tutizame mashindano ya mchezo wa kuteleza barafuni yaliyofanyika Pekin China.Timu ya Gabriella Papadakis na Guillaume Cizeron kwa pointi 200.43 na kuvunja rekodi ya dunia.Timu hiyo hiyo ilipata pointi 119.33 katika mashindano ya bure.

 

Sasa tutizame mchezo wa tenisi

Roger Federer mchezaji tajiri zaidi katika ulimwengu wa tenisi.Federer amekuwa ni mchezaji anaelipwa zaidi katika mashindano ya ATP.

Federer milioni $109,853,682

Novak Djokovic milioni $ 109,805,403

Rafael Nadal milioni $ 91,199,322

 

Steff Graf,ni mchezaji anatambulika kuwa mahiri katika mchezo wa tenisi kwa wanawake.Amelazimika kukaa mbali na mashindano baada ya kujifungua.Hii imempa fursa Serena Williams 36 kuweza kuivunja rekodi katika mashindano ya 24 ya Grand Prix.Anasubiria tena katika mashindano Australia.

 

Mashindano ya pikipiki 

Mashindano ya mwisho na muhimu kabisa ya pikipiki yamefanyika Qatar.Katika mashindano hayo ya mita 300 Lucas Mahias aliweza kumaliza wa kwanza na kuwa bingwa.Katika raundi ya mwisho Kenan Sofoğlu amemaliza katika nafasi ya tatu na wa pili katika duniani.

Sofoğlu hakuweza kushiriki katika baadhi ya mashindano kutokana na majeraha aliyokuanayo.

Matokeo yalikuwa kama hivi:

Bingwa Lucas Mahias 190 pointi

Kenan Sofoğlu 161

Jules Cluzel 155

Sherindan Morais 141

Na katika nafasi ya tano Federico Caricasulo 118

 

Tumtizame Felipe Massa ni mchezaji kutoka Brazil  ambae ameweza kuwa katika mashindano ya Formula 1 kwa miaka 15 ,kushinda katika mashindano 11, na kushiriki mara 41.Baada ya kuagana na mashindano hayo mchezaji mwenzake Valtteri Bottas alihamia timu nyingine na kumlazimu Massa kurudi uwanjani.Hata hivyo Felipe Massa mwenye umri 36 anaonekana kutobadili mawazo yake na kusimamia uamuzi wake wa kutorudi uwanjani.

Ulimwengu wa michezo daima hauna mwisho.

 Habari Zinazohusiana