Zambia na Cameroun walazimishana kwenda sare ya kufungana 2-2

Cameroun na Zambia wameenda sare ya kufungana 2-2 katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kwenda kombe la dunia Urusi 2018.

Zambia na Cameroun walazimishana kwenda sare ya kufungana 2-2

 

Cameroun na Zambia wameenda sare ya kufungana 2-2 katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kwenda kombe la dunia Urusi 2018. Mchezo huo umechezewa kwenye uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia. Ikumbukwe kuwa licha ya mchezo huo, nchi zote hizo hazina matumaini ya kwenda Urusi.

Chipolopolo waliliona lango la Simba wa Cameroun mnamo dakika ya 26 kupitia mchezaji Patson Daka, baada ya dakika 5 André-Frank Zambo Anguissa wa Cameroun akasawazisha goli hilo. Timu zote hizo mbili zilienda mapumzikoni wakiwa na goli 1-1.

Mnamo kipindi cha pili, Zambia iliingiza kwa mara nyingine tena goli la pili dakika ya 64 kupitia mchezaji Brian Mwila, lakini mda kidogo Cameroun wakaweza kujibu goli hilo kwenye kipindi cha majeraha mnamo dakika ya 90 kupitia Yaya Banana.

Baada ya mchezo huo,Zambia wamemaliza wakichukua nafasi ya 2 na pointi 8 huku Cameroun wakiwa nafasi ya 3 na pointi 7 katika kundi la B.

 Habari Zinazohusiana