Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Naim Süleymanoğlu

Hakuna maneno yanayotosha kumuelezea shujaa huyu

Ni mtu aliyeacha historia 

Alishinda ubingwa mara nane

Alivunja rekodi ya dunia mara arobaini na sita

Alikuwa bora katika mchezo wa kunyanyua vyuma

Ameacha historia nzuri

Hakuna mwisho wa sifa za bingwa huyu

Naim Süleymanoğlu ambae amevunja rekodi katika maisha yake ya wanamchezo duniani alipoteza maisha yake wiki iliyopita

Süleymanoğlu alizaliwa mwezi Januari 23. 1967.

Alianza mchezo wa kubeba vyuma akiwa na umri wa miaka 15

Alikuwa bingwa wa dunia alipokuwa na miaka 55

Aliweza kujishindia medali za dhahabu mbili wakati ana umri wa miaka 15

Alikuwa ni mbeba vyuma mwenye umri mdogo kabisa na alivunja rekodi kwa kuweza kubeba mara tatu vyuma vyenye uzito sawa na yeye

Baada ya hapo alijipatia ubingwa kwa kubeba vyuma vyenye uzito wa kilo 52,56,60.

Alichaguliwa kama mbeba vyuma wa dunia katika miaka ya 1984,1985,1986.

Alishinda Seoul 1988,Barcelona 1992,Atlanta Olimpics 1996.

Mnamo mwaka 1992 bodi ya kimataifa ya mchezo huo ilimchagua kama mbeba vyuma bora ulimwenguni.

Naim Süleymanoğlu alijipatia umaarufu katika historia ya michezo nchini Uturuki hasa baada ya kuwa mtu wa kwanza kushinda medali ya dhahabu baada ya kushindana katika olimpiki.

 

Tutizame mchezo wa mpira wa kikapu.Shirikisho la kimataifa la mpira wa kikapu FIBA imetoa uamuzi muhimu.Uamuzi huo ni hatua kubwa kwa timu pamoja na wachezaji wenyewe.Kwa yule mchezaji yoyote atakaepata jeraha katika mchezo,basi ataendelea kulipwa mshahara wake kama kawaida kipindi chote cha kutibu majeraha.Mpango huo umetiwa saini na FIBA na endapo mchezaji atafanyiwa Operesheni basi malipo yote ya matibabu yatalipwa na shirika hilo.

Mpango huu ni kwa wale wachezaji wanawake na wanaume walio na umri wa 17,18,19 na 20.

 

Tutizame mashindano ya Formula 1.

Michael Schumacher ni jina muhimu kabisa katika mchezo huu.Baada ya kuachana na mashindano ya magari ya Formula 1 ,Michael alianguka na kupiga kichwa wakati akiteleza katika theluji Ufaransa 29 Desemba 2013.

Anaendelea kupata matibabu nyumbani kwake Uswisi.

Japokuwa Schumacher hayuko katika mashindano hayo tena,gari alilotumia kujipatia ubingwa Monaco Grand Prix mwaka 2001 limepigwa mnada.

Gari hilo limenunuliwa kwa thamani ya dola za kimareni milioni 7,500,409.Aliyenunua gari hilo hakutaka jina lake litajwe hadharani.

 

Tutizame mashindano mengine ya magari nchini Australia.Wakati Thierry Neuville alijipatia ubingwa msimu uliopita,Sebastian Ogier ndie bingwa wa dunia wa sasa.Mashindano hayo yalifanyika Australia Coff Harbour ndani ya raundi 21 kwa kilomita 318.3.Thierry ameweza kumaliza kwa daraja 2.35.44.8 akiwa wa kwanza.

Ott Tanak amechukua nafasi ya pili,Hayden Paddon nafasi ya tatu.

Matokeo yalikuwa kama hivi:

1.Sebastian Ogier 232 pointi

2.Thierry Neuville 208

3.Ott Tanak 191

4.Jari Matti Latvala 136

5.Elfyn Evans 128

 

Tutizame mashindano ya tenisi ya ATP

Grigor Dimitrov amekuwa bingwa

Katika mashindano yaliyoshirikisha wachezaji bora nane wa mchezo huo,fainali ilichezwa kati ya Grigor Dimitrov na David Goffin mjini London.

Katika seti ya kwanza ya mchezo iliyochukua saa moja na nusu Dimitrov alishinda kwa 7-5.Katika seti ya pili alishinda Goffin 6-4 na katika seti ya mwisho Dimitrov alishinda kwa 6- 3 na kujinyakulia ubingwa.

Hio ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wachezaji hao kukutana fainali na mara ya nane kwa mchezaji Dimitrov kupata ubingwa.

 

Ulimwengu wa michezo daima hauna mwisho.

 Habari Zinazohusiana