Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Mihraç Akkuş amechaguliwa kama mchezaji bora wa judo katika mashindano ya vijana ya Ulaya.Mihraç Akkus amechaguliwa katika nafasi ya tatu kwenye tuzo zilizotolewa na Piotr Nurowskı mwaka huu.Jambo hilo limemfanya aonekana bingwa.

IAAF imechagua mwanamke na mwanaume bora katika riadha.Katika hafla iliyoandaliwa Monacco ,Essa Bashir kutoka Qatar ndiye amechaguliwa kama mwanariadha bora katika wanaume hasa baada ya kujishindia medali ya dhahabu katika mashindano yaliyofanyika London.
Nafissiatou Thiam kutoka Ubelgiji ndiye amechaguliwa mwanariadha bora katika wanawake hasa baada ya kujishindia medali ya dhahabu.Ramil Guliyev nae alihudhuria hafla hiyo.

Maandalizi ya mashindano ya mhula mpya wa mchezo wa tenisi yanaendelea.Toni Nadal,ni kati ya watu muhimu kabisa katika mafanikio ya Rafael Nadal.Toni Nadal ni mjomba na kocha wa Rafael Nadal.Baada ya kuwa katika fani hiyo miaka 27,kocha huyo ametangaza kuachana na kazi hiyo.Toni Nadal ametoa shukrani zake za dhati kwa Rafael Nadal na kusema kuwa ameenda sehemu nyingi nzuri,akakutana na watu wengi wazuri na kufanya mambo mengi mazuri akiwa pamoja na Rafael Nadal.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 56,amekuwa muhimu kwa Rafal kushinda mashindano ya 16 ya Grand Slam na kupata ubingwa wa 75.
Kwa upande mwingine wachezaji kama Andy Murray na Ivan Lendi wametoa shukrani zao za dhati kwa kocha huyo na kusema kuwa wamejifunza mengi.
Mnamo mwaka 2012 na 2014 Lendi alifanya kazi na Murray na kushinda mashindano ya Marekani pamoja na yale ya Wimbledon na kujipatia medali ya dhahabu.Amelia Mauresmo baada wa Ufaransa alirudi tena kufanya kazi na Lendi baada ya kuwa ameondoka.

Jana Novotna aliyekuwa bingwa katika mashindano ya Wimbledon ya wanawake amepoteza maisha akiwa na umri wa miaka 49 kutokana na ugonjwa wa saratani.Alijipatia umaarufu sana hasa baada ya kushinda katika mashindano ya Wimbledon ya mwaka 1998.

Mashindano ya msimu wa baridi na theluji ya FIS kwa mara ya tatu yatafanyika Erciyes.Itakua na mchezo wa kuteleza katika barafu wa kilomita 115.

Mchezaji Oscar Pistorius ambae alikuwa mlemavu wa kwanza kushindana katika mashindano ya olimpiki ameongezewa adhabu ya kifungo na mahakama ya Afrika Kusini baada ya kumuua mchumba wake mnamo mwaka 2013.
Hapo awali alipewa kifungo cha miaka 6 jela kabla ya kuomba kupewa kifungo cha nyumbani.Miaka ya kufungwa imeongezwa kuwa 13.

Tutizame mashindano ya mpira wa kikapu.Timu za Fenerbahçe na Anadolu zipo katika ligi ya Ulaya.Katika kombe la Ulaya kutakuwa na timu za Darüşşafaka,Tofas,FİB,Gaziantep na Banvit.
Katika ligi ya ulaya,Fenerbahçe Doğuş imechukua nafasi ya tatu huku Anadolu Efes ikiwa nafasi ya 15.
Katika kundi A kuna Gaziantep,kundi D Tofaş,Kundi B Galatasaray na kundi C Banvit.

Tutizame timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya Uturuki.Timu hiyo imechukua nafasi ya pili baada ya kuishinda Ukraine 67-60.Timu ya Uturuki iliweza pia kuishinda Norway 82-73 pamoja na Latvia 85-73.

Mashindano ya Formula 1 ya 20 na ya mwisho yamemalizika Abudabi.Japokuwa mashabiki walijua ubingwa utachukuliwa na Lewis Hamilton,haikuwa hivyo.Valtteri Bottas ndie amejinyakulia ushindi.Katika mashindano ya mita 5554 ndani ya raundi 15 kwenye uwanja wa Yas Marina,Lewis Hamilton amechukua nafasi ya pili,Sebastian Vettel ya tatu.
Felipe Massa 36 ambae ameshika nafasi ya kumi,ametangaza kuachana na mchezo huo.Felipe amekuwa katika mashindano hayo kwa muda wa miaka 16.
Matokeo yalikuwa kama hivi:
Bingwa ni Lewis Hamilton 
2.Sebastian Vettel 317 pointi 
3.Valtteri Bottas 305
4.Kimi Raikkoken 205
5.Daniel Ricciardo 200.

Ulimwengu wa michezo hauna mwisho.Sent from my iPhoneHabari Zinazohusiana