Ligi ya Uingereza yamalizika kiaina yake.

Hatimaye Mechi 38 za msimu huu za ligi maarufu duniani,EPL zimemalizika, huku kila timu ikivuna ilichopanda.

Ligi ya Uingereza yamalizika kiaina yake.

Hatimaye Mechi 38 za msimu huu za ligi maarufu duniani,EPL zimemalizika, huku kila timu ikivuna ilichopanda.

 

Manchester City wao wameibuka vinara wa ligi hiyo kwa kujikusanyia alama 100, baada ya kushinda michezo 32, timu ya kwanza kupata alama hizo na kushinda idadi hiyo katika historia ya ligi ya Uingereza. 

 

Manchester United na Tottenham zimemaliza katika nafasi ya pili na ya tatu, zikijihakikishia kushiriki  Klabu bingwa barani Ulaya. Huku Liverpool ikishika nafasi ya 4 na kwenda kwenye mitoano ya klabu bingwa. 

 

Kwa Mara ya kwanza baada ya miaka mingi kudumu ndani ya ligi hiyo, Stoke city imejikuta ikienguliwa katika ligi hiyo pamoja na timu za Swansea na West Brom. 

 

Mabingwa wa msimu uliopita, Chelsea wamejikuta wakitupwa nje na kushika nafasi ya tano, hivyo itashiriki kombe la Europa baadaye mwaka huu.  

Arsenal wao wameambulia patupu baada ya kuangukia nafasi ya 6 ya mashindano hayo.


Tagi: Uingereza , ligi

Habari Zinazohusiana