Mo Salah ndio habari ya mjini EP

Mo Salah amekua mchezaji wa kwanza wa  kufikisha Magoli 32 ndani ya msimu mmoja katika EPL katika historia ya ligi hiyo.

Mo Salah ndio habari ya mjini EP

Mshambuliaji nyota wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohammed Salah amekua gumzo nchini Uingereza na duniani kwa ujumla baada ya kufanikiwa kuvunja rekodi kedekede ndani ya ligi hiyo. 

Mo Salah amekua mchezaji wa kwanza wa  kufikisha Magoli 32 ndani ya msimu mmoja katika EPL katika historia ya ligi hiyo. 

Awali rekodi hiyo ilikua inashikiliwa na Alan shearer, Chriastiano Ronaldo na Luis Suarez ambao wote walifanikiwa kufunga Magoli 31 katika msimu mmoja. 

 

Aidha "the Egyptian King" amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu akimpiku  Kevin De Bruyne wa Manchester City. 

Mo Salah pia amekua tishio katika klabu bingwa barani Ulaya ambapo amefanikiwa kuweka kimyani Magoli 10 na kuipeleka Liverpool fainali za madhindano hayo huku akipata tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kwa Mara 4. 

Licha ya kucheza msimu mmoja tu ndani ya Liverpool, Mo Salah amekua ndiye mchezaji alofanikiwa kufunga Magoli mengi zaidi ndani ya msimu mmoja wa EPL  katika historia ya klabu hiyo. Na kwa sasa Mo  Salah anashika nafasi ya pili kwa Magoli ya mashindano yote ndani ya msimu mmoja Liverpool. 

Endapo atafanikiwa kuweka kimyani Magoli 3, basi atakua mchezaji nambari moja. 

 

Nyota huyo tayari ameshinda kiatu cha dhahabu cha ligi ya Uingereza, huku akiwa nyuma ya Lionel Messi pekee katika idadi kubwa ya Magoli barani Ulaya.Habari Zinazohusiana