Rais Erdoğan ampongeza Cristiano Ronaldo

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan ampongeza nyota wa kabumbu wa Ureno Cristiano Ronaldo kwa msimamo wake kuhusu wapalestina

Rais Erdoğan ampongeza Cristiano Ronaldo

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan ampongeza nyota wa kabumbu wa Ureno Cristiano Ronaldo  kuhusu  msimamo wake na wapalestina.

Rais wa Uturuki ametoa pia  pongezi kwa nyota huyo  kutokana na uchezaji wake anapokuwa  uwanjani.

Akiwa katika  hafla ilioandaliwa  katika  kituo cha mafunzo ya urubani na anga, rais wa Uturuki amezungumza na vijana kuhusu maendeleo na teknolojia.

Wakizungumzia kuhusu kombe la dunia Urusi, rais Erdoğan amesema kuwa  timu ambazo  zilikuwa zikiwekewa matumaini na kuonekana kuwa ni timu kubwa zinakabiliwa na upinzani mkubwa.

Rais Erdoğan amesema kuwa  alikuwa akidhani kuwa Ujerumani  inashinda katika mechi  yake ya kwanza na kushangazwa na matokeo. Yalioikuta Brazil tunayafahamu sote amesema rais Erdoğan.

Alipouulizwa kuhusu  Cristiano Ronaldo na  Lionel Messi, rais Erdoğan  amepongeza uchezaji wa  Ronaldo katika mechi iliomalizika kwa mabao matatu kwa tatu.

Rais Erdoğan amempongeza pia Ronaldo kwa msimamo wake kuhusu wapalestina.Habari Zinazohusiana