Özil na Gündoğan watuhumiwa kusababisha Ujerumani kuondoka mapema kombe la dunia

Mesut Özil na Ilkay Gündoğan watuhumiwa kuhusika na kuondoka mapema kwa timu ya Ujerumani katika michuano ya kombe la dunia

Özil na Gündoğan watuhumiwa kusababisha Ujerumani kuondoka mapema kombe la dunia

Mesut Özil  anaechezea  kalbu ya Uingereza na timu ya taifa ya Ujerumani pamoja na mwenzake Ilkay Gündoğan ambae pia anachezea klabu ya Manchester City  Uingereza  wanatuhumiwa kuwa sababu iliopelekea timu ya taifa ya Ujerumani kuondoka mapema katika michuano ya  kombe la dunia la FIFA mwaka 2018 nchini Urusi.

Baadhi ya viongozi nchini Ujerumani  wanawatuhumu wachezaji hao wenye  asili ya Uturuki kuwa sababu ilioplekea timu ya Ujerumani kufungwa na kuondoka mapema katika michuano ya kombe la dunia.

Kwa mujibu wa viongozi hao, wachezaji kabumbu hao wawili mwenendo waliokuwa nao hivi karibuni  ni moja ya sababu ya Ujerumani kufungwa na kuondoka katika michuano mapema.

Picha waliopiga wakiwa na rais wa Uturuki   katika ziara yake nchini Uingereza ilizua gumzo na kashfa dhidi ya wachezaji hao wenye asili ya Uturuki.

 Habari Zinazohusiana