Man U yarudi kwa kishindo, yashinda 3-2

Newcastle walijiandikia goli la kwanza mnamo dakika ya 7 ya mchezo.

Man U yarudi kwa kishindo, yashinda 3-2


Mashetani wekundu kutoka katika jiji la Manchester walitolewa jasho na Newcastle United katika mchezo wa ligi kuu ya Mechi ilianza kwa kasi na bila kulaza damu, Newcastle walijiandikia goli la kwanza mnamo dakika ya 7 ya mchezo.

Fumba na kufumbua, Vijana hao wa Benitez waliongeza goli la pili mnamo dakika ya 12 ya mchezo, magoli ambayo yalidumu mpaka mwisho wa kipindi cha kwanza. 


Baada ya kuona jahazi linazama, Mourinho aliamua kufanya mabadiliko katika kikosi chake na kuwaingiza wachezaji 4 kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji. 


Juan Mata alichukua nafasi ya Bail, huku Alexis Sanchez akiingia kuchukua nafasi ya Rashford na Fellain akiingia kuongeza nguvu katika safu ya kiungo. 


Mabadiliko hayo yalianza kuzaa matunda mnamo dakika ya 70 ya mchezo ambayo Juan Mata alifanikiwa kuifungia Man U goli la kwanza kwa mpira wa adhabu ulio nje kidogo ya eneo la hatari. 


Antonio Martial aliiweka sawa Man U kwa hilo lake mahiri la kusawazisha kabla ya Alexis Sanchez kupigilia msumari wa mwisho katika jeneza la New castle na kupelekea mechi kuisha 3-2. 


Dakika 20 za mwisho za mchezo zimeiokoa Man U na kuiwezesha kutwaa point tatu zote muhim.Habari Zinazohusiana