Bonaventure Kalou achaguliwa kuwa Meya mpya jiji la Vavoa

Bonaventure Kalou achaguliwa kuwa Meya mpya jiji la Vavoa nchini İvory coast

Bonaventure Kalou achaguliwa kuwa Meya mpya jiji la Vavoa

Mchezaji wa zamani wa İvory coast Bonaventure Kalou amechaguliwa kuwa meya wa jiji la Vavoa linalopatikana katikati mwa nchi hiyo.

Mchezaji huyo wa zamani wa vilabu vya PSG,Auxerre na Feyenoord alichaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jumamosı iliyopita, kwenye uchaguzi huo Kalou alishiriki kama mgombea binafsi.

“Najivunıa sana na napata hisia za baba yangu ( aliefariki mwaka 2016)  ambaye alipenda sana kuwa meya wa eneo hili nafuata nyayo zake ,”Alisema baada ya kutangazwa mshindi.

Meya Kalou ataongoza jiji lenye idadi ya watu wanaokadiriwa kufikia nusu milioni, Sensa ya mwisho iliyofanyika eneo hilo ilikuwa ni mwaka 2014 na kulikuwa na watu 400 000.Habari Zinazohusiana