Mashindano ya marathon ya New York yafanyika

Simbu, Kamworor washindwa kufua dafu New York marathon, 2018 Keitany na Desisa waibuka washindi

Mashindano ya marathon ya New York yafanyika

Mashindano ya marathon ya New York yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu kubwa yamefanyika.

Kwa upande wa wanaume mwanariadha kutoka Ethiopia Lelisa Desisa aliibuka mshindi wa kwanza kwa kutumia muda wa masaa 2 dakika 5 na sekunde 59 kumaliza, kwa wanawake Mary Keitany ameweka rekodi mpya kwa kuibuka mshindi wa kwanza kwa mara ya nne mfululizo.

Mashindano hayo ambayo yalianzia Staten Island, yalimalizikia Central Park. Mkenya Geofrey Kamworor ambaye ameshawahi kushinda mbio hizo aliibuka mshindi wa nne. mtanzania Erick Simbu hakufua dafu kwenye mbio hizo.

 Habari Zinazohusiana