Barca waibuka kidedea Messi akifikifisha magoli 400

Timu ya soka ya Barcelona imeendelea kubaki kileleni baada ya kupata ushindi wa goli 3 kwa nunge dhidi ya Eibar

2019-01-13T191630Z_1160173873_RC13191DD450_RTRMADP_3_SOCCER-SPAIN-FCB-EIB.JPG
2019-01-13T185952Z_45032159_RC1EFB0152B0_RTRMADP_3_SOCCER-SPAIN-FCB-EIB.JPG

 

Katika wiki ya 19 ya ligi kuu ya Uhispania (La Liga), Barcelonaikicheza uwanja wa nyumbani imefanikiwa kupata ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Eibar.

Magoli hayo ya Barcelona yalipatikana dk 19 na dk 59 kupitia kwa Luis Suarez ambaye ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo.

Lionel Messi naye aliipatia goli Barcelona dk ya 53, goli hilo linamfanya nahodha huyo wa Barcelona kufikisha magoli 400 katika michezo 435 ya La Liga aliyoingia dimbani tangu ajiunge na timu hiyo msimu wa 2004-2005.Habari Zinazohusiana