Uhamisho wa mwaka
Real Madrid yavunja vibubu kumnasa Eden Hazard
Real Madrid watoa ofa ya pound milioni 100 kumnunua kiungo wa Chelsea raia wa Ubelgiji, Eden Hazard.
Kwa mujibu wa habari iliyochapishwa na gazeti la Telegraph, Timu hiyo ya Uhispania inamtaka nyota huyo wa Chelsea na imeshatangaza dau la pound milioni 100 kumnasa kiungo huyo.
Chelsea wamethibitisha kupokea ofa hio. Akizungumza na redio ya Ufaransa RMC, Hazard alisema Hajui atakachofanya ila ameshafanya maamuzi.
Hazard ambaye aliwahi kusema alikuwa na ndoto za kuichezea Real, sasa inaonekana kwamba ndoto yake hiyo itatimia mwisho wa msimu.