Mwili uliotolewa ndani ya bahari wathibitishwa kuwa wa mchezaji kabumbu Emeliano Sala

Mwili uliotolewa ndani ya bahari  baada ya ndege kufanya ajali wathibitishwa kuwa mwili wa mchezaji kabumbu Emeliano Sala ambae alikuwa akichezea timu ya Cardiff City

Mwili uliotolewa ndani ya bahari  wathibitishwa kuwa wa mchezaji kabumbu  Emeliano Sala

Mwili uliotolewa ndani ya bahari  baada ya ndege kufanya ajali umethibitishwa kuwa mwili wa mchezaji kabumbu mwenye asili ya Argentina Emeliano Sala ambae alikuwa akichezea timu ya Cardiff City.

Polisi ya uchunguzi imethibitisha kuwa mwili uliopatika baada ya ajali  ya ndege iliotokea Januari 21 ni muili wa  mchezaji huyo.

Mwili uliookolewa Februari 6 na kuchunguzwa kitaalamu  katika kisiwa cha Portland umethibitishwa kuwa wa Sala.
Mabaki ya ndege aliokuwemo hayakuweza kuondolewa bahari kutokana na hali mbaya ya hela .
Emeliano Sala alikuwa amesaini makubaliano na timu ya Cardiff City kwa  thamani ya Pound milioni 15.Habari Zinazohusiana