Hikaya za Anatolia

Hikaya za Anatolia

Hikaya za Anatolia

Leo katika hikaya za Anatola tutatizama mji wa Eskişehir.Mji huo ni maarıfu katika kutengeneza zawadi na vitu vya thamani kwa kutumia mawe meupe na mazuri .

Tutizame je ni vipi mawe hayo yalipatikana ?

Hapo zamani za kale,kulikuwa na kijana aliyekuwa akitembea katika jua kali akitokea kijijini kuelekea mjini.Safari yake ilikuwa ni ndefu na hivyo basi alikuwa  akipumzika na kisha akaamua kukaa na kupata mlo aliyokuwa ameubeba kutoka nyumbani.Alikula mkate pamoja na maji ya kunya na kisha akashtukia amepitiwa na usingizi.Wakati akiendelea kufurahia usingizi wake alishtushw na sauti ya gurudumu dogo kama mpira lililokuwa na rangi nyeupe ya kuvutia.Jiwe hilo lilifanana na barafu na hivyo kumvutia kijana yule kutokana na joto alilokuwa akiskia.

Alilisogelea jiwe lile na kulitizama kwa kina.Na kisha akalichukua mkonononi na kutoa kisu kilichokuwa ndani ya mfuko wake wa suruali.Alianza kulichomachoma jiwe lile kwa kutumia kisu.Alikuwa na nia ya kuliweka katika umbo zuri.Mara tu jiwe likamponyoka na kuanguka chini.Jiwe likaongea na kusema, ‘Unantakia nini kijana wewe kunichoma choma ?.Nilikuwa nimekaa vizuri ukaanza kunichoma choma na kisu chako.

Kijana alipigwa na butwaa.Ni vipi jiwe linaweza kuongea.Wakati bado akiendelea na mshangao huo,ghafla jiwe lilibadilika na kuwa binti mzuri wa ajabu.Huo ukawa ni mshangao wa pili kwani hakuweza kuamini kuwa jiwe limegeuka kuwa binti mrembo.Wakati bado akishangaa.binti mrembo alirudi tena katika umbo la jiwe na kudunda mpaka jiwe hilo likadumbukia katika tundu moja.Kijana alipagawa na kulikimbilia akitizama kama ataona chochote katika shimo lile.Hakuona chochote.Akaanza kuchimba kwa nguvu zote akiwa na nia ya kumuona binti yule kwa mara nyingine.Siku zilizidi kwenda na kijana anachimba tu.Alichimba mpaka akachoka,haoni kitu.Wanakijiji wakazipata habari na ghafla wakajikusanya na wao wakitaka kusaidia katika uchimbaji huo.Walichimba na kuchimba mpaka wakataka kukata tamaa.Mara ghafla wakaona mawe meupe na mazuri mengi.Hawakujua nini maana ya mawe hayo.Wao walikuwa wakimtaka binti.Walipoona hamna kilichobakia,walianza kukusanya mawe hayo meupe na kuyatengenezea vitu mbalimbali kama vile zawadi na kadhalika.

Mpaka wa leo mji wa Eskişehir unajulikana kwa utengenezaji wake wa zawadi zenye thamani.Eskişehir ni mji ambao upo karibu na Ankara pamoja na Istanbul hasa baada ya kuanzishwa usafiri wa treni.Wanafunzi wengi hujikusanya mahala hapo na kununua zawadi mbalimbali.

Tukutane tena juma lijalo kwa hikaya motomoto za Anatolia.Habari Zinazohusiana